Tanzania imezizima, dunia imetaharuki kwa kuwa Magufuli alifanya yale wanadamu waliyotarajia kama kiongozi. Je, yupo atakayeweza kuvaa viatu vyake?

Hakuna chochote cha msingi kilicho tofauti alichofanya Magufuli ambacho hakikufanywa na Sokoine.

Na inawezekana Sokoine alifanya yote aliyoyafanya Magufuli bila vituko visivyo na staha vya Magufuli.

Na wote wawili walikosea kwa kutaka kuongoza kibabe bila kuheshimu kanuni za msingi za uchumi.
 
You do not understand how governments around the world are run and operate,na kwa bahati mbaya you believe anything you hear,huna diagnostic ability na akili ya kujiongeza,sikulaumu.
 
Sina sababu ya ku-argue na a programmed,mind controlled and an enslaved individual Kiranga,that is who you are.I like people who think independently.
 
Sina sababu ya ku-argue na a programmed,mind controlled and an enslaved individual Kiranga,that is who you are.I like people who think independently.
Huna sababu ya ku argue au huwezi ku argue?
 
Rekodi nyingine ngumu kuvunja ni:
~Kupiga hoja kwa risasi.
~Kuua watu.
~Kupiga marufuku siasa.
~Kujilinda kwa kutumia marcenaries.
~Kupora wafanyabiashara.
~Kuzurura na mabulungutu ya fedha za kugawa kama takrima.
~Kudumaza taasisi na mihimili ya dola

Mengine ya sijuhi ujenzi wa nini au kusimamia nini na nini ni majukumu ambayo kiongozi yeyote ni lazima afanye...!!
 
Ka-google maana ya dictator ujifunze zaidi.Labda swali la kujiuliza ni why Magufuli and not Nyerere or Mkapa.It's a simple question, but sensible.
 
Wadanganywe wale wanaoandamana kuaga mwili lakini siyo sisi na akili zetu. Huyu ametawala kwa PROPAGANDA na mwisho wa PROPAGANDA ni tarehe 26/ 03/ 2021 tukisha MFUKIA.

Huyu Magufuli ametembea kwenye misingi iliyojengwa na MKAPA na KIKWETTE Ila watangulizi wake hawakuwa watu wa MISIFA
 
Kwani amefanya nini???
 
Ukijikita kwenye propaganda unageuka kuwa mjinga kwa watu wenye uelewa. Wakati wa Nyerere tuliambiwa hatuwezi kupata rais kama Nyerere, leo hii mnatuambia hatuwezi kupata rais kama Magufuli! Hivi mbona mnatuchanganya, au nyie ndio mmechanganyikiwa?
Hivi unajua tumepita miongo mingapi kupata kariba ya Rais kama Nyerere?kumpata mwanasiasa kariba ya Magufuri sio leo,wakina Magufuri wanazaliwa wachache sana.R.i.p Magufuri ulikuwa Rais wa pekee Africa imepoteza mtu.
 
Tupate tena muuaji, mtekaji, mtesaji na mwenye roho mbaya kama magu?
Wewe naona umezaliwa jana tu, niambie Rais gani ambaye ajaua ktk utawala wake?titajie kuanzi kwa Nyerere mpaka kwa Kikwete,hata huko ulaya mnako sema kuna democlasia hukijifanya kichwa ngumu unaondoka na maji,akuna democrats isiyo na mipaka,uwezi vurunga nchi watu watu wakakuangalia tu.
 
Hivi unajua tumepita miongo mingapi kupata kariba ya Rais kama Nyerere?kumpata mwanasiasa kariba ya Magufuri sio leo,wakina Magufuri wanazaliwa wachache sana.R.i.p Magufuri ulikuwa Rais wa pekee Africa imepoteza mtu.

Kabla ya yeye kuingia madarakani deni la taifa lilikuwa 39t+, leo deni la taifa ni 59t+ yaani ametengeneza 1/3 ya deni la marais wote wanne wa kabla yake. Miradi yake mikubwa miwili ya SGR na SG(JNHPP) inakadiriwa kufikia 15t+ hakuna hata mmoja uliofikia nusu ya matarajio. Sasa hapo jipime hilo deni la 20t limefanya miradi gani ya kufikia kiwango hicho?
 
Jaribu kuweka na kasoro zake Kama binadamu pia
 
You do not understand how governments around the world are run and operate,na kwa bahati mbaya you believe anything you hear,huna diagnostic ability na akili ya kujiongeza,sikulaumu.
Kwa hiyo ben sa8, mawazo, azory nk walistahili kufa kwa sababu hawakukubaliana dikteta? Lissu alistahili kufa sababu ya kupinga udikteta? However, God is great, he's gone at last
 
Bwana Yesu alisema: "Kweli nawaambieni, anayeniamini atafanya mambo ninayofanya mimi; naam, atafanya hata makuu zaidi..." (Yohane 14:12). Kama haya maneno ya Yesu ni ya kweli, ina maana kama tulimwamini JPM na kuamini aliyofanya kwa ajili yetu, 'tutafanya aliyoyafanya na hata makuu zaidi'. Kama tulifanya 'lip service' ni wazi kwamba tutashindwa. Hivyo, jibu lake unalo wewe na mimi na yule na yule kule na wao na wengine wale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…