Tanzania ina mambo ya ajabu sana; Uhamiaji inanyima watu wanaotusaidia uchumi work permits, wanapofunga ofisi na kuaga Serikali inawaomba wasiondoke!

Kuna mmoja alikuwa anafanya kazi shirika la afya Ireland! Aliomba managament ya shirika hili lisaidie kujenga hospitali kijijini kwetu na iwe full equips mpaka CT SCAN akakubaliwa! lakini alipoanza kutafuta kibali alijibiwa serikali imejitosheleza! Siku hizi hata kuja kutalii haji tena anaenda zake South tu!
 
Hapana Mkuu. Kumbuka hii ofisi inahusiana na University hivyo wanaonyimwa permit ni wale wataalamu wanaokuja kwa ajili ya kufanya mafunzo. KUmbuka kwamba kwa utaratibu wa Tanzania, chukulia kama shirika la ndege KLM kwa mfano, ndege yao ikiharibika Tanzania pale JKNIA, ili mainjinia wao waje kutoka Netherlands kuitengeneza say kwa siku 7, wanahitaji work permit.

Kwa hiyo hata kama hawa wataalamu say magwiji wa University hii kutoka Canada wangekuwa wanakuja nchini kuendesha mafunzo bado watahitaji work permit. Hata mwandishi wa habari akija toka nje kufanya covering ya wiki moja serikali yetu inataka awe na work permit.

Sasa kuzipata hizo work permit, acha za muda mrefu, hata za muda mfupi tu ni issue kali Tanzania

Mkurugenzi aliwekwa Mtanzania kwa hiyo na yeye anapoteza kazi
 
Hii nchi ni ya vituko mno,permits zote zilitakiwa zitolewe na uhamiaji this buck stop on their door,ila wizara ya kazi inatoa mapendekezo yake kwa uhamiaji kuhusu umuhimu wa mtu anayeombewa permit,kwa nchi zinazojielewa wana kitu kinaitwa critical skills,sasa watu wenye nazo hizi ili kupata permit inabidi wapate motivation letter kutoka kwao,ila ni uamuzi wa immigrations wa kumpa au kukataa.tuendelee kusubiri noah zetu pale KIA.
 
Nimekuelewa sana mkuu....
na inatia sana uchungu....
niliwahi lalamika pahala...
 
Work permit inatolewa na wizara ya kazi ukimaliza unaenda uhamiaji kupata resident permit ilitakiwa kuwe na dirisha moja la kushugulikia hayo Mambo vinginevyo usumbufu unabaki palepale
 
 
Halafu pia na ikumbukwe kuwa Tanzania haitoi kitu kinaitwa permanent residence permit. Wanakataa katakata, si kwa wale waliooa au kuolewa Tanzania, hata wawekezaji walioajili Watanzania na ambao wamekuwa Tanzania kwa zaidi ya miaka mitano. Nchi nyingi duniani ukishakuwa na residence au work permit kwa zaidi ya miaka mitano ukiishi katika hiyo nchi, basi unakuwa ume-qualify kupata Permanent Residence Permit. Tanzania hakuna mtu anapewa permanent residence permit labda kwa maagizo ya Magufuli tu.
 
Work permit inatolewa na wizara ya kazi ukimaliza unaenda uhamiaji kupata resident permit ilitakiwa kuwe na dirisha moja la kushugulikia hayo Mambo vinginevyo usumbufu unabaki palepale
Okay sawa. Hata hivyo ujinga na upumbavu katika suala hili unabaki pale pale hata kama waliofanya hivyo ni Wizara ya Kazi
 
Kama unayemsaida hataki msaada wako si unaondoka tu. Tushakuwa matajiri, au hamsikii kila siku mkubwa akisema
 
Work permit inatolewa na wizara ya kazi ukimaliza unaenda uhamiaji kupata resident permit ilitakiwa kuwe na dirisha moja la kushugulikia hayo Mambo vinginevyo usumbufu unabaki palepale
Hebu ona hapa. Work permits za Tanzania zinaitwa Residence Permits Class A, B na C. Na zinatolewa na Uhamiaji. Hata ukinyimwa una appeal kwa Waziri Mambo ya Ndani, sio Wizara ya Kazi

 
Kama unayemsaida hataki msaada wako si unaondoka tu. Tushakuwa matajiri, au hamsikii kila siku mkubwa akisema
Mkuu huyo asiyetaka msaada ni Tanzania au watendaji wajinga na wapumbavu ndani ya Tanzania? Mie ni Mtanzania nahitaji huu msaada, sasa nani anasema sitaki msaada? Huyo aliyekaa ofisini ndio anahitaji huu msaada?
 


Whatever lakini wamenyimwa

Wewe utuambie unajaribu kutetea nini?
 
Nasikia Rwanda watu kama hawa wanapewa kila kitu hadi ulinzi
 
WOte ni wapumbavu hao walikuwa wanatengeneza mazingira ya rushwa.

Hawana lolote walimuacha isabela ameenda ubelgiji amerudi na korona wapo wapo tu na inabidi hii korona iwakamte wampelekee hata bosi wao ili wakoma na watie akili
Corona ianzie kwao na familia zao mtu kaondoka sijui tar 5/3 -15/3 karudi wakati huko mambo si mambo ,chakushangaza waliwazui wanafunzi wasirudi vyuoni wala walioko huko wasirudi huyo sijui aliwapa nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ulivyoiweka ni as if work permit ndio sababu pekee ya hawa kuondoka.
Hats km kungekuwa na sababu 1000, lkn work permit ikawa moja wapo ya sababu, lzm serikali ione kwamba ina mchango wake na imawajibika kujenga mazingira rafiki
 
We jamaa ni zuzu
 
.

Huu ndio kati ya urasimu ambao unadidimiza ukuaji wa kiuchumi nchi hii. Kwanini mtu anayetaka kufanya kazi nchi hii alazimike kutafuta permits mbili? Hivi mtu akipewa work permit halafu anyimwe residence permit itakuwaje? Maana huwezi kufanya kazi nchini bila kuwa resident.

Mimi nadhani kwa wafanyakazi wageni permit ingekuwa moja, yaani uhamiaji na wizara ya kazi wangeungana wakatoa permit moja ambayo utaratibu wa kuipata ungekuwa mmoja. Ili mtu akishaipata anaanza kazi moja kwa moja.

Residence permit za uhamiaji zibaki kuwa za waliooa/kuolewa na watanzania. Na mtu ambaye ni mke/mume wa mtanzania na wanaishi nchini automatically angeruhusiwa kufanya kazi na angepewa ukaazi wa kudumu (permanent residence) na baada ya miaka kadhaa angeruhusiwa kuomba uraia. Huu ndio utaratibu unaotumiwa na nchi nyingi tu duniani sijui kwanini sisi tunajiona wapekee sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na mapungufu huku immigration, nadhani kuna suala zito zaidi nyuma ya pazia. Awamu hii haina mwamko na NGO kwa vile wanataka kudhibiti kila kitu. NGO wanakuwa huru na miradi na fedha zao ambazo hazipiti jungu kuu na hivyo kujikuta wanakuwa frustrated na system.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…