Wakati mwingine ukifikiria maamuzi ya watendaji wa nchi hii yatakushangaza.
Kwa mfano: Bunju mwisho stand ya mabasi, walikuja wakasema mabasi yatoke yawe yanapaki barabarani watengeneze barabara na stand. Imepita zaidi ya miezi mitatu hakuna matengenezo ya stand wala nini na magari yanaendelea kupaki barabra ya Bagamoyo na kusababisha foleni.
Sasa kama walijua hawakuwa tayari, kwanini waliondoa mabasi hayo.
Na wafanyabiashara waliokuwa wamechukua mabanda pale stand kwa sababu hakuna biashara abiria hawaingii stand nao wamehamia barabarani.
Hii inanikumbusha walipobomoa stand ya Ubungo wakati ya Magufuli ilikuwa haijawa tayari na kusababisha abiria kupata shida sana.
Mfano 2: Siku moja Rais alikuwa anaenda Wazo kwa Makamba Sr. Siku 3 kabla wakapitisha gereda kurekebisha barabara ya mtaa maana ilikuwa ni mbovu sana. Wakaondoa vibanda vilivyo karibu na barabara. Bodaboda wakaambiwa kituo wakiondoe wakae mbali kabisa na barabara.
Rais akaja hata nusu saa hakukaa akaondoka maisha yakarudi kama kawaida. Sasa mimi kilichonishangaza haya ya kuondoa mabanda na boda wakae mbali walitaka Rais asione maisha halisi ya raia wake? Ina maana rais hajui uhalisia wa maisha ya raia wake na anapaswa asijue?
Kuna vitu vinafikirisha kweli