Tanzania inaelekea wapi? Hili ni swali zuri la kujiuliza kwa wale wote wanaoitakia mema nchi hii. Sijasoma makala, kama ipo, kuhusu swali hili kwamba serikali inaelekea wapi.
Pamoja na hayo nitoe mchango wangu kidogo. JIBU la jumla kwa swali hilo na kwa kuzingatia hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi iliyopo nchini kwa sasa ni kwamba TANZANIA INAELEKEA KUZIMU.
Tanzania ya sasa siyo ile ya miaka ya 1960 ambapo wananchi walikuwa na matumaini makubwa ya maisha bora ya baadaye baada ya ukoloni. Wala tanzania hii siyo ya miaka ya 1970 au 1980. Tanzania ya sasa ni ya wananchi waliokata tamaa; wavivu; wapiga majungu; na walafi wa kupindukia.
Mtu (aliyeko kwa nafasi ya ulaji) anajilimbikizia bilioni 20 lakini shule zetu ziwe na primary aju sekondari au hata vyuoni hakuna vifaa vya kutosha. Rushwa imetawala kila mahali. Huna pesa sasa na unaumwa ni lazima utakufa tu. Huwezi kutibiwa Muhimbili au hospitali yoyote ile ya serikali na siku hizi hata za binafsi bila kutoa rushwa.
Watanzania ni wavivu, inherently wavivu, siyo wachapa kazi wakiwa hapa Tanzania. Makampuni ya nje yakija hayapendi kuajiri watanzania kwa kuwa ni wavivu na wapiga majungu wakuu. Kwenye maeneo ya kazi vyama vya wafanyakazi (Trade unions) kazi yao ni kutetea wavivu na majungu. Trade unions zinajifanya zinatetea haki lakini kimsingi zinatetea uozo uliopo nchini mwetu kwenye maeneo ya kazi.
Dar es salaam ni jiji chafu kupindukia lisilo na nidhamu kwa upande wa wakazi wake. Kila mtu ni mjanja. Dereva wa gari anaweza akasimama katikati ya barabara na kuanza kupiga soga na wengine na wala asijue kuwa kwa kufanya hivyo anasababisha foleni na adha kwa wengine. Na hata akisababisha foleni atafanywa nini?
hakuna anayewajibika tanzania kila mtu ni mjanja. Tuna mawazo bado ya kinyama kwa kutostarabika. Tanzania ilivyo sasa inahitaji dikteta au utawala wa sheria za kijeshi ili kutuwaajibisha. Demokrasia ya vyama vingi vya siasa ni ujinga mtupu. Kila muda ni siasa siasa siaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaasa tu.
Wanasiasa wanawazia uchaguzi tu. Mtu ameitumbukiza nchi hii kwenye matatizo lakini bado ana mawazo ya urais mwaka 2015 au hata 2010. Vyombo vya habari ndiyo usiseme, waandishi wa habari au tuseme wahariri wana misimamo yao au mtu wao. Fulani anaweza kuwa fisadi kwa gazeti au redio fulani lakini huyo huyo anaweza kuwa mtu safi kwa gazeti au chombo kingine cha habari.
Magazeti yanaanzishwa kwa kuwaandama watu wengine na kuwasafisha watu wengine. Waandishi wa habari hawawezi tena kuwakomboa watanzania kwani nao ni mafisadi. Yaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani tuko matatizoni. Tunaelekea kuzimu. Nothing is working in this country. Magazeti yamekaa kuandika umbea tu. No serious analysis on serious issues. Every thing is taken lightly.
Rwanda inatupita kimaendeleo na sisi tumekaa tu. Burundi nayo itakwenda kwenye maendeleo sisi tunakazania kuimba wimbo usio na tija kwamba eti Tanzania ni nchi ya amani. Iko wapi hiyo amani na mshikamano au umoja wa kitaifa kama sio utani wa karne?