Tanzania inafuata Kalumekenge system!?

Tanzania inafuata Kalumekenge system!?

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Posts
1,135
Reaction score
130
We can take a story of Kalumekenge as a system of accountability in any government system.
The story is as follows:
Once upon time Kalumekenge alikataa kwenda shule. Fimbo ikaambiwa imchape Kalumekenge kwa sababu Kalumekenge amekataa kwenda shule.Fimbo ikakataa kumchapa Kalumekenge. Moto ukaambiwa uichome Fimbo kwa sababu imekataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule.Moto ukakataa kuichoma Fimbo. Maji yakaambiwa yauzime Moto kwa sababu Moto umekataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Maji yakakataa kuuzima moto. Mbuzi akaambiwa ayanywe Maji yaliyokataa kuuzima Moto uliokataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Mbuzi alikubali kuyanywa maji yaliyokataa kuuzima Moto uliokataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Baada ya Mbuzi kukubali kuyanywa Maji. Ndipo Maji yalikubali kuuzima Moto. Moto ukakubali kuichoma Fimbo. Fimbo ikakubali kumchapa Kalumekenge. Kalumekenge akakubali kwenda shule.

Ofcourse hii ni hadithi ya kitoto lakini maudhui yake ni ya ki-utawala na uwezo wa uthubutu aliyenao kiongozi mmoja mmoja ndani ya mfumo wa ki-utawala.

Ukirejea kwenye story hii utaona kwamba chain ilianzia kwa kiongozi mmoja katika jamii asiyetaka kuwajibika (Kalumekenge) pamoja na kuyajua na kuyakubali majukumu yake katika jamii.

Lakini kwa kufahamu mfumo aliomo ni wa ki-shkaji hautaweza kumchukulia hatua yoyote kwa kukataa kwake majukumu yake (kwenda shule) kwa makusudi na bila sababu.

Hili linajidhihirisha pale alipotokea kiongozi mmoja mwenye uthubutu (Mbuzi) mfumo wote ulikwenda sawa kwa kuwa kila mtu anafahamu majukumu yake, ila watu wanakwepa kuwajibika kwa kuwa utamadumi wa uwajibikaji umeingiliwa na virusi hatari miongoni mwa viongozi wa leo.

Hadithi hii na itukumbushe jinsi ambavyo mifumo yetu muhimu ilivyo paralize na kupelekea maadili ya viongozi kuporomoka. Na kuacha wananchi tukilalamika: Mafisadi,EPA, Richmond etc.

TUMTAFUTE WAPI MBUZI ili MAHAKAMA,BUNGE NA SERIKALI ziweze kufanya kazi ipasavyo na kupelekea TAKUKURU,DPP,BOT na idara zingine zinazo fanana za serikali zinazofanana na hizo ziweze kufanya kazi ipasavyo na kutupa raha WANANCHI?

NAWASILISHA.
 
Mhh....
Umenikumbusha mbali saana.
Sijui nitapata wapi kitabu chenye hadithi hiyo
ya kalumekenge kwa faida ya watoto wa siku hizi
ambao wanajua kutazama tamthilia tu basi...
 
Usisahau kwamba hiyo ndiyo kazi ya MAKTABA.
 
Maktaba ipi?
Kitabu kinaitwaje na kimeandikwa na nani?
Mi hiyo hadithi niliisikia kwa mdomo tu.
Kinauzwa wapi?
 
We can take a story of Kalumekenge as a system of accountability in any government system.
The story is as follows:
Once upon time Kalumekenge alikataa kwenda shule. Fimbo ikaambiwa imchape Kalumekenge kwa sababu Kalumekenge amekataa kwenda shule.Fimbo ikakataa kumchapa Kalumekenge. Moto ukaambiwa uichome Fimbo kwa sababu imekataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule.Moto ukakataa kuichoma Fimbo. Maji yakaambiwa yauzime Moto kwa sababu Moto umekataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Maji yakakataa kuuzima moto. Mbuzi akaambiwa ayanywe Maji yaliyokataa kuuzima Moto uliokataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Mbuzi alikubali kuyanywa maji yaliyokataa kuuzima Moto uliokataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Baada ya Mbuzi kukubali kuyanywa Maji. Ndipo Maji yalikubali kuuzima Moto. Moto ukakubali kuichoma Fimbo. Fimbo ikakubali kumchapa Kalumekenge. Kalumekenge akakubali kwenda shule.

Ofcourse hii ni hadithi ya kitoto lakini maudhui yake ni ya ki-utawala na uwezo wa uthubutu aliyenao kiongozi mmoja mmoja ndani ya mfumo wa ki-utawala.

Ukirejea kwenye story hii utaona kwamba chain ilianzia kwa kiongozi mmoja katika jamii asiyetaka kuwajibika (Kalumekenge) pamoja na kuyajua na kuyakubali majukumu yake katika jamii.

Lakini kwa kufahamu mfumo aliomo ni wa ki-shkaji hautaweza kumchukulia hatua yoyote kwa kukataa kwake majukumu yake (kwenda shule) kwa makusudi na bila sababu.

Hili linajidhihirisha pale alipotokea kiongozi mmoja mwenye uthubutu (Mbuzi) mfumo wote ulikwenda sawa kwa kuwa kila mtu anafahamu majukumu yake, ila watu wanakwepa kuwajibika kwa kuwa utamadumi wa uwajibikaji umeingiliwa na virusi hatari miongoni mwa viongozi wa leo.

Hadithi hii na itukumbushe jinsi ambavyo mifumo yetu muhimu ilivyo paralize na kupelekea maadili ya viongozi kuporomoka. Na kuacha wananchi tukilalamika: Mafisadi,EPA, Richmond etc.

TUMTAFUTE WAPI MBUZI ili MAHAKAMA,BUNGE NA SERIKALI ziweze kufanya kazi ipasavyo na kupelekea TAKUKURU,DPP,BOT na idara zingine zinazo fanana za serikali zinazofanana na hizo ziweze kufanya kazi ipasavyo na kutupa raha WANANCHI?

NAWASILISHA.
Safi saana!
 
"mbuzi" wapo wengi sasa. tatizo ni wananchi wenyewe. chukuli mfano wa sekta kama elimu:

unaitishwa mgomo kwa ajili ya kushinikiza kulipa madai ya walimu yaliyolimbikizwa, lakini unakuta baadhi ya walimu wanendelea kufundisha baada ya kuambiwa madai yake yanahakikiwa!

wakina mrema wakati wakiwa serialini wangeweza ufananishwa na "mbuzi" lakni walipothubutu kunywa maji hawakupata uungwaji mkono wa kutosha, leo mnawacheka kuwa wamefuli! kumbe ni sisi wenyewe hatukuwaunga mkono.

ukiitisha maandamano ya kumpongeza m/kiti wa ccm kwa hotuba nzuri hta kama unafahau wazi kuwa si hotuba aliyoandika mwenyewe, yeye alikuwa anasoma tu, imeandikwa na wengine! usishangae kukuta barabaa zimefungwa kwa wingi wa watu,

akina slaa wametuambia vizuri mpaka wametutajia majina ya wabaya wetu, sasa itisha maandamano ya kumuunga mkono slaa uone utapata watu wangapi!

nk, nk, nk......

hitimisho:
kwa maoni yangu, hiyo nadharia yako haifanyi kazi tanzania
 
mbuzi wa sikuhizi wanaogopa kunywa maji....
na wengine wanaanza kunywa maji halafu wakifika katikati kabla maji hayajaisha wanatamani majani.
 
ndiyo maana nasema hiyo nadharia haifanyi kazi tanzania
 
Asante sana mkuu jayfour_king hii story very interesting ukweli kwa bongo kupatikana
mbuzi kazi sana kutokana na uwelewa wa demokrasia kwa wanajamii za kitanzania wa
bongo wanadhani demokrasia ni amani hata kama mambo ya msingi ya kitaifa hayaendi sawa nadhani sasa tuanze kumtafuta mbuzi hata kama ni wajirani haje kunywa maji mambo yaende otherwise tutaumizwa sana
 
Boss kitabu hicho sidhani kama kinachapishwa tena kwa sasa. Ilikuwa ni series za vitabu vinaitwa "Someni kwa furaha".

Kitabu hicho pia kilikuwa na hadithi kama za "Nchi ya Wagagagigikoko" na nyengine za kufurahisha watoto na kusaidia mtoto kusoma maneno magumu. Mimi nilisoma kitabu hicho 1966 (yes!) nilipokuwa darasa la tatu.

Hii ni out of context na hiyo mada iliyopo hapo juu lakini najaribu kujibu suali la Boss.
 
boss kitabu hicho sidhani kama kinachapishwa tena kwa sasa. Ilikuwa ni series za vitabu vinaitwa "someni kwa furaha".

Kitabu hicho pia kilikuwa na hadithi kama za "nchi ya wagagagigikoko" na nyengine za kufurahisha watoto na kusaidia mtoto kusoma maneno magumu. Mimi nilisoma kitabu hicho 1966 (yes!) nilipokuwa darasa la tatu.

Hii ni out of context na hiyo mada iliyopo hapo juu lakini najaribu kujibu suali la boss.

nashkuru,thanx
 
"mbuzi" wapo wengi sasa. tatizo ni wananchi wenyewe. chukuli mfano wa sekta kama elimu:

unaitishwa mgomo kwa ajili ya kushinikiza kulipa madai ya walimu yaliyolimbikizwa, lakini unakuta baadhi ya walimu wanendelea kufundisha baada ya kuambiwa madai yake yanahakikiwa!

wakina mrema wakati wakiwa serialini wangeweza ufananishwa na "mbuzi" lakni walipothubutu kunywa maji hawakupata uungwaji mkono wa kutosha, leo mnawacheka kuwa wamefuli! kumbe ni sisi wenyewe hatukuwaunga mkono.

ukiitisha maandamano ya kumpongeza m/kiti wa ccm kwa hotuba nzuri hta kama unafahau wazi kuwa si hotuba aliyoandika mwenyewe, yeye alikuwa anasoma tu, imeandikwa na wengine! usishangae kukuta barabaa zimefungwa kwa wingi wa watu,

akina slaa wametuambia vizuri mpaka wametutajia majina ya wabaya wetu, sasa itisha maandamano ya kumuunga mkono slaa uone utapata watu wangapi!

nk, nk, nk......

hitimisho:
kwa maoni yangu, hiyo nadharia yako haifanyi kazi tanzania
Kwa melezo yako mkuu, inaonysha kwamba wananchi HATUJAIVA elimu ya uraia matokeo yake hatujioni kuwa na nguvu ya mwajiri (ambayo ki-kweli tunayo) na badala yake tunaishi tukiwaongopa na kujipendekeza kwa waajiriwa wetu (viongozi) hata pale wanapofanya makosa ya wazi. Wanalifahamu hili na wanalitumia ipasavyo (kwa faida yao).

Wito sasa: Inatakiwa tutoke humu chumbani na tuanzishe phisical forums kama moto uliowashwa na MWALIMU NYERERE FOUNDATION.
 
Back
Top Bottom