Jayfour_King
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 1,135
- 130
We can take a story of Kalumekenge as a system of accountability in any government system.
The story is as follows:
Once upon time Kalumekenge alikataa kwenda shule. Fimbo ikaambiwa imchape Kalumekenge kwa sababu Kalumekenge amekataa kwenda shule.Fimbo ikakataa kumchapa Kalumekenge. Moto ukaambiwa uichome Fimbo kwa sababu imekataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule.Moto ukakataa kuichoma Fimbo. Maji yakaambiwa yauzime Moto kwa sababu Moto umekataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Maji yakakataa kuuzima moto. Mbuzi akaambiwa ayanywe Maji yaliyokataa kuuzima Moto uliokataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Mbuzi alikubali kuyanywa maji yaliyokataa kuuzima Moto uliokataa kuichoma Fimbo iliyokataa kumchapa Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Baada ya Mbuzi kukubali kuyanywa Maji. Ndipo Maji yalikubali kuuzima Moto. Moto ukakubali kuichoma Fimbo. Fimbo ikakubali kumchapa Kalumekenge. Kalumekenge akakubali kwenda shule.
Ofcourse hii ni hadithi ya kitoto lakini maudhui yake ni ya ki-utawala na uwezo wa uthubutu aliyenao kiongozi mmoja mmoja ndani ya mfumo wa ki-utawala.
Ukirejea kwenye story hii utaona kwamba chain ilianzia kwa kiongozi mmoja katika jamii asiyetaka kuwajibika (Kalumekenge) pamoja na kuyajua na kuyakubali majukumu yake katika jamii.
Lakini kwa kufahamu mfumo aliomo ni wa ki-shkaji hautaweza kumchukulia hatua yoyote kwa kukataa kwake majukumu yake (kwenda shule) kwa makusudi na bila sababu.
Hili linajidhihirisha pale alipotokea kiongozi mmoja mwenye uthubutu (Mbuzi) mfumo wote ulikwenda sawa kwa kuwa kila mtu anafahamu majukumu yake, ila watu wanakwepa kuwajibika kwa kuwa utamadumi wa uwajibikaji umeingiliwa na virusi hatari miongoni mwa viongozi wa leo.
Hadithi hii na itukumbushe jinsi ambavyo mifumo yetu muhimu ilivyo paralize na kupelekea maadili ya viongozi kuporomoka. Na kuacha wananchi tukilalamika: Mafisadi,EPA, Richmond etc.
TUMTAFUTE WAPI MBUZI ili MAHAKAMA,BUNGE NA SERIKALI ziweze kufanya kazi ipasavyo na kupelekea TAKUKURU,DPP,BOT na idara zingine zinazo fanana za serikali zinazofanana na hizo ziweze kufanya kazi ipasavyo na kutupa raha WANANCHI?
NAWASILISHA.