Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

Mleta mada nikuulize yule Mkuu wa wilaya aliyeteuliwa enzi za mwandazake akafika hadi ukumbini kwa ajili ya kula kiapo na muda mfupi akatolewa kwamba sio yeye je ulimwanzishia uzi? Au umeona kuwa sasa uko huru hata kutaja majina ya watu humu jukwaani tena kwa kijinasibu kuwa unajiamini? Leta hiyo thread humu nijue una msimamao tangu mwanzo.
 
Hapo kwenye umri umechemka, rais wa sasa wa US ana miaka mingapi?
Mwache Mama achape kazi, hayo ni mambo madogo yatarekebika with time.
 
Wabongo mna vipaji vya kulalamika , kulaum na unafiki.

Mama wewe chapa kazi ukiona Shida mahali itatue papo hapo.

Ulidhani mama anashindwa kuwaacha hao walioteuliwa bahati mbaya waendelee kuchapa kazi mpaka baadae kabisa Kama wakina Kitwangwa?

Anachokifanya Rai's anakifanya Kwa nia njema kabisa.
 
Siku zote marais wastaafu wanakuwa ni sehemu ya washauri wa marais waliopo madarakani. Hii ipo dunia nzima. Mzee Biden pamoja na kuwa anamzidi Obama miaka 19 lakini kwa Obama kumtangulia kuwa rais tayari ni sehemu ya washauri wake muhimu na wa karibu.

Urais ni cheo kikubwa sana, na Mzee Kikwete ni mwanadiplomasia mzoefu, hivyo kwa Rais Samia kumkwepa ni suala lisilowezekana. Kikwete ni muhimu kwa Samia kwa sasa kuliko wakati wowote ule.

Rais wa sasa ni mwanamke wa kwanza kuongoza Tanzania, hawezi kufanya baadhi ya maamuzi kama ambayo yangefanywa na rais mwanaume. Ni kumvumilia na kumtia moyo.
 

Tukisema akina warumi, tunaonekana sukuma Gang... raisi hatuna hapa kwa kweli
 
"Hayati Rais Dkt. Magufuli alikuwa na ' Mapungufu ' yake ila nilikuwa nikimpenda zaidi katika tabia yake ya kupenda Kujiridhisha, Kudadisi, Kufuatilia Jambo na kufanya Maamuzi ya uhakika ambayo huenda yakachelewa ila hayatotupa Mashaka na kuanza Kutusababishia tuwe na Maswali mengi."

Hayo maneno yako ndio Usukuma Gang wenyewe. JPM huyu huyu aliyemini Kabudi Nguli wa sheria anafaa Mambo ya nje na Mahiga Nguli wa diplomasia anafaa sheria?

Pia tambua kwamba hakuna haja ya kutoa mfananisho wa Samia mtoto Pwani , mtoto wa mjini na JPM aliyekulia porini akichunga ng'ombe akaishia kuwa mshamba wa madaraka.

Umakini wa Kiongozi ni kuchukua hatua papo hapo ili mradi anafanya hivyo Kwa nia njema.
 
Kama mwendazake ndiye alikuwa na sifa ambazo mama hana. Ni kheri mno mama azikose kabisa.

Mama akaze uzi hapo hapo tayari dawa inapenya.

Uzi gani sasa akaze? Anahangaika tu na maisha
 
Ukiona mpaka kigwangala anaanza kujipendekeza kwa kikwete, unapata picha kuwa watu sio wapumbavu, wanajua wanachokifanya
Hahaha mambo ya CCM nawaachia CCM wenyewe, tangu watuidanganye kuhusu ile 50m kwa kila kijiji na Laptop kila mwalimu nimeamini kuwa mkweli ni Pombe tu, wengine wote waongo tu
 
Rais ana majukumu mengi hivyo kutimiza yote bila kuwa na wasaidizi wenye weredi kutakuwa hakuna tija ndio maana teuzi zipo na zinazingatia sheria zote

Kitendo cha kumsema mzee JK kuwa ndo anashika kalamu bila ushaidi huu ni uzandiki mkuu mbona kipindi Mzee JPM alipokuwa karibu sana na hayati BWM hukuja na uzi wa kumshauri? Leo Mama pia kafanya lile lile kama la JPM kuwa karibu na BWM yeye kawa karibu na Jk sasa ndo imekuwa udwazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…