Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

Nafasi ya uraisi imemuangukia tu hakujiandaa kwa majukumu hayo mazito ya kazi ya lawama. sidhani kama ni sawa kuendelea kumjudge bado ana mengi ya kujifunza. Japokua binafsi naona still she is a weak president.

Very weak indeed, mpaka anatia hasira sana , yani yupo yupo kazubaa utadhan msukule wa kimbiji, yani haeleweki siku hadi siku
 
Wabongo mna vipaji vya kulalamika , kulaum na unafiki.

Mama wewe chapa kazi ukiona Shida mahali itatue papo hapo.

Ulidhani mama anashindwa kuwaacha hao walioteuliwa bahati mbaya waendelee kuchapa kazi mpaka baadae kabisa Kama wakina Kitwangwa?

Anachokifanya Rai's anakifanya Kwa nia njema kabisa.

Kazi gani sasa anayoifanya? Mi sijaona bado
 
Kwa maoni yangu nadhani ni kuwa rais ameanza kwa kupanga na kupangua kikosi kazi kwaajili ya kuendana na misimamo yake.

Yani ni kama kocha mpya akichukua team lazima kuna panga pangua huwa zinatokea kwenye kikosi ikiwamo na sajili mpya na kutemwa baadhi ya wachezaji ili kocha abaki na wale ambao wata fit kwenye mfumo wake.

Baada ya siku 100 madarakani kama hizi panga pangua hazijaisha basi nami nitakuunga mkono mleta mada.

Mada yako ina hoja nzito lakini.
Shida siyo panga pangua, kateua yeye mwenyewe halafu kabla ya kuapisha mteule anatengua Tena!! Is this right?
 
Give her a break! Also, she has a right to choose her advisors based on own criteria. At the end of the day "the Buck Stops at Her Desk"
You must be an authentic 'Moron' on JF.
 
Mtaanza sasa Kutulazimisha kuamini kuwa Watu wa Jinsia fulani si ' Competent ' kwa nafasi ya ' Head of State ' na akina GENTAMYCINE tukiamini hivyo msituchukie au msianze ' Kutubatiza ' Jina lenu la SUKUMA GANG mkimaanisha ni Wapinzani ' Tukuka ' wa Utawala huu wa Rais ( Mama ) Samia Suluhu Hassan.

Tanzania ya sasa inahitaji Rais ambaye haishii tu kuwa Mchapakazi bali pia mwenye uwezo wa Kufuatilia Jambo, Kusoma sana, Kujiridhisha na kuwa na Timu ya Wasaidizi ( Washauri ) wenye Akili hasa na siyo Wapumbavu wenye ' Uchawa ' mwingi.

Kibinadamu Tukio moja linasameheka kwani hata Mimi GENTAMYCINE na hata Wewe ' Member ' pia huwa tunakosea ila Mtu huyo huyo akilirudia tena Tukio ( Kosa ) hilo hilo anaanza kututia Mashaka na kuanza kutupa Mtihani mzito wa Kumjibia kutoka kwa wale wasiomkubali.

Nina mengi Moyoni na Rohoni ila kabla tu Hasira zangu hazijanipanda zaidi kwa Upuuzi unaoanza Kuzoeleka natoa Ushauri wa bure kwa wale Watanzania ambao watagombea Urais miaka ijayo GENTAMYCINE nawaombeni teueni Makamu wa Rais Vijana ( Damu Changa ) na pia wawe ' very intelligent ' ili hata ikitokea Mmekufa ( Mmefariki ) watakaotwaa Madaraka ' Kikatiba ' wawe ni Watu ambao hawatotupa Mashaka Mashaka katika Kuwaamini kama ninavyoanza kupata Mashaka hayo sasa.

Najua kwa Uzi huu leo nami nitabatizwa kuwa natokea SUKUMA GANG hivyo nikiitwa hivyo kwa kusema huu Ukweli wangu nitalipokea hilo Jina ila pamoja na kwamba Hayati Rais Dkt. Magufuli alikuwa na ' Mapungufu ' yake ila nilikuwa nikimpenda zaidi katika tabia yake ya kupenda Kujiridhisha, Kudadisi, Kufuatilia Jambo na kufanya Maamuzi ya uhakika ambayo huenda yakachelewa ila hayatotupa Mashaka na kuanza Kutusababishia tuwe na Maswali mengi.

Mlio karibu na Mheshimiwa Rais nanyi pia ni sehemu ya tatizo kwani hamumsaidii hadi Mama kila mara anatoa ' Maboko ' yake tu ya ' Kuteua Kutengua ' au yawezekana pia mkawa katika Mpango ' Maalum ' wa Kumpigisha Shoti ( Kumuhujumu Mama ) ili aharibikiwe na achekwe Yeye na tuchekwe pia Sisi wana CCM wote.

Mwisho namalizia kwa Mama ( Mheshimiwa Rais ) hebu punguza sana kuwa karibu kwa 99% na Rais Mstaafu Kikwete ( hasa Kiushauri ) kwani Kitendo hiki ' Kinawakera ' baadhi ya Watendaji wako ( tena Waandamizi kabisa ) na usipokuwa nacho makini kitakuja Kukugharimu na utakuja Kunikumbuka GENTAMYCINE niliyenyimwa Utajiri na Nguvu ila niliyepewa Fikra na Maono na Mwenyezi Mungu.

Sisemi usimsikilize Mzee Kikwete bali acha Kumfanya ndiyo kila Kitu Kwako Kiushauri bali Shirikisho pia na Watu ( Wastaafu ) wengine lakini pia Waamini na hao Watendaji wako ulionao sasa Serikalini kwani huenda na Wao wakawa na Mawazo Cbanya Kwako Kimaendeleo na Kiuongozi hata kuliko hayo unayoyapata kwa Mzee Kikwete.

Hii ' Teua Tengua ' iwe mwisho Mama!!!!
Unaonekana una hoja muhimu lkn unapayapaya mwisho una haribu. Una ushahidi gani kuwa Mheshimiwa Rais anamtegemea Mzee Kikwete katika maamuzi yake? Una uhakika gani Mheshimiwa hapewi ushauri wa kurosha na wasaidizi wake? Ni mapema sana kuelekeza tuhuma nzito kwa Mheshimiwa Rais. Sisi wengine tunamuamini na tunamuona kuwa yupo kwenye right truck. Kama nawe upo kwenye"... gang ulilolitaja, tulia dozi ikuingie vizuri".
 
Kuwa na kiongozi ambaye anafanya teuzi halafu ndani ya muda mfupi anafanya utenguzi kabla ya wateuliwa aliowapitisha kuapishwa kuna shida mahali, hii inaonesha ni kwa jinsi gani mama si msomaji ama mfuatiliaji mzuri wa mambo.

Kuna shida mahali kwa washauri wa mama, pia namshauri aongeze umakini sana kama anaanguka mapema kwenye masuala ya uteuzi, je ataweza kuongoza taifa kweli?

Kuna kitu hakiko sawa kwa huyu kiongozi wetu
Binafsi ana shida na hana Washauri pia.
 
Kwa maoni yangu nadhani ni kuwa rais ameanza kwa kupanga na kupangua kikosi kazi kwaajili ya kuendana na misimamo yake.

Yani ni kama kocha mpya akichukua team lazima kuna panga pangua huwa zinatokea kwenye kikosi ikiwamo na sajili mpya na kutemwa baadhi ya wachezaji ili kocha abaki na wale ambao wata fit kwenye mfumo wake.

Baada ya siku 100 madarakani kama hizi panga pangua hazijaisha basi nami nitakuunga mkono mleta mada.

Mada yako ina hoja nzito lakini.
Kwani misimamo yake imetofautiana na mwendazake? Mbona alikuwepo enzi hizo, na alikuwa na team hiyo? Basi nakuja kuamini kile kilichokuwa kinasemwa kuhusu the close relationship ya mzee wa Msoga na Madame.
 
Umeongea point kabisa kiukweli hata mm binafsi ningependa kumuona Rais Samia akifanikiwa na mafanikio yake ndiyo mafanikio ya Tanzania tatizo linakuja anapokubali kushikiwa kalamu kwenye kuandika anatakiwa asiendekeze urafiki kwenye mamlaka aliyonayo ni makubwa mnoo inabidi awe na utulivu wa hali ya juu sana katika kufanya maamuzi akiendekeza undugu na urafiki safari kwake itakuwa ngumu ayavae mamlaka ya Urais awe na mipaka atengeneze mazingira ya kutozoeleka zoeleka
Apunguze sana Uswahili, Uvivu na Soga.
 
Back
Top Bottom