Kuna jambo ambalo nimekuwa nikilitafakari kuhusu mfumo wetu wa uongozi.
Katika nchi yoyote, rais ni kiongozi mkuu wa nchi. Lakini je, maendeleo ya nchi yanapaswa kutegemea uwezo na utashi wa mtu mmoja au uimara wa taasisi za nchi?
Tuchukulie mfano: Rais akiamua jambo fulani, je, taasisi husika zinapaswa kutekeleza bila kuhoji, au zinapaswa kuwa na uwezo wa kutoa ushauri, kukosoa na kusimamia sheria?
Tunaweza kuwa na rais mzuri leo, lakini je, tutahakikisha tunapata mfumo mzuri hata kesho atakapoondoka?
HOJA ZA KUJADILI:
Je, rais anapaswa kuwa na mamlaka makubwa kiasi gani?
Je, Bunge lina uhuru wa kutosha kuisimamia serikali?
Je, mahakama zinapaswa kuwa huru kiasi gani?
Je, watumishi wa umma wanapaswa kuwa na uhuru wa kutoa ushauri unaopingana na maamuzi ya viongozi?
Ni kipi muhimu zaidi: kiongozi bora au taasisi imara?
Ningependa kusikia mitazamo tofauti. Tusibishane kwa majina ya watu, tubishane kwa hoja, mifano na ushahidi.
TANZANIA INAHITAJI NINi HASA?