Haya ya kweli kuwa hakuna chanzo.. maana tunaweza tukazama kuzungumzia ufisadi tukaacha mambo yanayogusa maisha ya watu wa kawaida kama haya. Naomba taarifa wa ndugu ili tumtafute Waziri anayehusika na Afya. kina Domokaya naomba mniandikie kwenye PM ni vituo gani hivyo mlivyoenda na kama kuna mtu ana contacts za waganga wakuu wake... haitoshi kulalamika tu ni lazima tufanye kitu.
ndugu yangu Mwanakijiji asante kwa kuonyesha kuguswa ha hii topic, mwanangu anapataga chanjo kwenye clinic moja ninaitwa FURAHA KWA PR. MASAWE na number yao ya simu ni hii +255 222 667 693, wewe piga na ulizia tu kama chanjo zimeshafika na utapata jibu zuri kuwa chanjo hakuna hata kwenye bohari kuu hawana kabisa..... leo hii nimetoka kupiga simu kuulizia na jibu nililopewa ni kwamba bado hazijaja na hawajui lini zitakuja,
Baadhi ya Hospital nilizotembelea kutafuta chanjo ni kama ifuatavyo:
1. Furaha clinic
2. Lugalo hosp. ya Jeshi.
3. Muhimbili.
4. Mnazi mmoja pale wanapotoa chanjo za kitaifa.
5. Gerezani hosp ya wilaya.
6. Kifuma.
na zingine nyingi nasikia hata huko mikoani chanjo zimekwisha kabisa, mimi nashangaa sana kikwete na wizara ya Afya wanafanya nini.
ukishakuwaondoa hawa utamuweka nani? ni vyema ukafikiria kabla ya kuwaondoa.washaondoka watatu kabla yake na hali haijawahi kubadilika. inabidi watanzania tutafute mbinu mpya sasa. tukaeni tufikiri.Sasa ni wakati wa kuamka, watanzania tukatae upuuzi huu njia ni kuungana pamoja na kuiondoa hali hii kwa kuwaoondoa madarakani.Napendekeza kwa kuanza tuwe na maandamano ya amani kuwaoomba wang'atuke !!