Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
jamani, jana nilipata mshituko wa ajabu, nilikwenda pharmacy moja nikakutana na akina mama wawili wanatafuta gloves eti wametumwa na zahanati ya "KIWANJA MPAKA" iliyoko soko matola Mbeya kuwa wakatafute hivyo vifaa kwa ajili ya ndugu yao anaetarajia kujifungua. Kwa bahati mbaya katika duka hilo gloves zilikuwa zimekwisha wakachanganyikiwa- walikuwa hawajui waende wapi saa tatu na nusu usiku. Hii haingii akilini? Gloves za shilingi mia mbili hazipo?
Pole sana ndugu yangu. CCM wamekandamiza Bilioni mbili na ushehe leo tu! Ndio Maisha Bora hayo ya Captain wa mafisadi.
Hilo Mafisadi hawalioni kwa sababu watoto wao hata wakijikwaa dressing ya Donda inafanyiwa nje ya nchi.
Kwahiyo hawawezi kuliona hilo kama ni tatizo maana haliwagusi moja kwa moja.
Hii nchi uhuni mwingi sana. Tusubiri vitengeMimi pia ni muhanga wa tatizo hilo. maaskini kabinti kangu kana miezi miwili chanjo kamepata juzi maana zilifika alhamisi. Domokaya kacheki hospital. Wamaiba pesa hata za chanjo kufanyia kampeni za chama. ama kweli hata laana za vichanga hivi washazipata. halafu utawasikia kila kukicha eti wana prevent mortality rate kwa under five years. Non sense.