Tanzania inampiga Ufaransa kama Ngoma

Tanzania inampiga Ufaransa kama Ngoma

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
U17 WWC 2022.
France 0-2 Tanzania 60'

====

TANZANIA imeonyesha uimara katika michuano ya Kombe la Dunia Wasichana U17 baada ya kuwachapa Ufaransa mabao 2-1 leo katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Jawaharlal Nehru, Margao, Goa nchini India.

Mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Diana Mnally dakika ya 16 na Christer Bahera dakika ya 56 kwa penalti, wakati la Ufaransa limefungwa na Lucie Calba dakika ya 75 na sasa watateremka tena dimbani Jumanne kukamilisha mechi zao za Kundi D kwa kumenyana na Canada.

Ikumbukwe Serengeti Girls ilianza vibaya michuano hiyo kwa kuchapwa 4-0 na Mabingwa watetezi, Japan.
 
Huyu keeper wa Tanzania aongezwe posho.
 
Hii timu inapata red card kila mechi?
Bahati mbaya lakini kupiga one of the biggest football nations in the world ni shangwe. Tunamsubiri Canada Jumanne Sisi ma under dog.
 
Katika michuano hii, mechi zangu bora hadi sasa ni Morocco Vs Brazil, na Marekani Vs Brazil. Morocco walifugwa 1-0 lakini waliupIga sana. Marekani na Brazil ilikuwa 1-1, lakini ilikuwa kama unaangalia gemu ya wanaume. Niko likizo hivi nazifaidi mechi zote, Supersport 224 na 225. Halafu wale wa Morocco ni Waislamu lakini sikuona hijab Hadi kwa makocha wao. Ila hivi vitoto vya kike vizuri sana aisee, naenjoy sana kuvitazama
 
Back
Top Bottom