Tanzania inamuhitaji Jaoa De Havelange katika soka, Jamal Malinzi ni chaguo sahihi.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Mpira wa Miguu, pia uitwao Soka au Kandanda ni aina ya mchezo wa mpira ambapo timu mbili za wachezaji kumi na mmoja hushindana kwa kupigania umiliki wa mpira na kuingiza mpira katika wavu wa wapinzani Wachezaji hucheza kwa miguu; pia wanaruhusiwa kutumia sehemu nyingine za mwili ila mikono hairuhusiwi kutumiwa. Mlinda mlango ndiye anayeruhusiwa kutumia mikono. Wachezaji wengine wanaweza kutumia mikono iwapo mpira ni wa kurushwa baada ya kutoka nje ya uwanja.

Naam shirikisho la mpira wa miguu duniani limepitia vipindi vingi na vigumu sana katika ramani ya ulimwengu,

Wale wanaofuasilia kwa karibu siasa za soka duniani hawatoshangaa ninapomtaja Havelange kama kiongozi mashuhurialiyeongoza shirikisho hili la FIFA kwa mda mrefu zaidi duniani,

Kuongoza kwamda mrefu hakukuja kwa hila wala bahati mbaya wala bahati nzuri bali uthabiti wa uongozi wake vilikuwa tu mbele ya wajumbe 2004 wa FIFA wenye dhamana ya kuchagua kiongozi wa chombo hicho dunia,

Jaoa De Havelange alikuwa ni mtu mwenye msimamo katika kazi na hakuendrshwa wala kutetereshwa na yeyote,

Katika kitabu chake kiitwacho 'How the Stole the Game', Havelange anasema kuwa yeye katika utendaji ndani ya fifa hakutetereshwa wala kumhofia yeyote,

Anasema "katika maisha yangu mtu ambae ningepeana miadi na nikamsubiri mahali angalau kwa dakika kumi ni Papa wa Roma na Malkia wa Uingereza tu"

Anasema wengine ilikuwani lazima wafuate sheria na kanuni za fifa na kuheshimu mda na ahadi,

Hivyo ni vibyagizo tu vya wasifu wa Mzee Havelange,

Tukirejea katika siasa za soka la bongo ambalo kimsingi linakua kwa mang'amung'amu ya bahati tu, hakika tunamhitaji mhafidhina wa kweli atakaetuongoza katiks kilele cha ubora wa soka halisi,

Nimetafakari kwa kina sana katika siku hizi chache zilizosalia kuelekea uchaguzi mkuu ndani ya shirikisho letu la mpira wa miguu TFF,

Katika wagombea wa nafasi ya urais yupo Jamal Malinzi na Athuman Nyamlani


Kama taifa linahitaji mageuzi ya kweli katika soka la dunia ya leo basi tuwaambie wajumbe wa wanaohusika na uchaguzi huu kuwa tunahitaji Havelange wa Tanzania,

Tunahitaji mtu ambae anauzoefu wa utawala wa soka, na tunahitaji mtu ambae yupo katika ulimwengu wa dunia ya tatu,

Hatutaki mtu atakaetumia tff kufanikisha biashara zake, hatutaki mtu atakaetumia tff kufanya biashara haramu hasa za madawa ya kulevya,


Jamal Malinzi amekuwa katika anga za soka kwa mda mrefu tena akihudumu katika ngazi ya juu kabisa ya soka nchini kupitia klabu,

Jamali Malinzi tunamjua fika kuwa ni mfanyabiashara halali wa shughuli za usafirishaji na ni mlipa kodi stahiki wa TRA,

Athumani Nyamlani simjui kwaundani katika anga la soka nchini, na sijui uhalali wa pato lake

Lakini ninachochojua nikuwa anaungwa mkono na genge la wezi
a matapeli nchini wakiongozwa na mtoto wa kigogo wa ccm,

Dhamira yao kuu ni kuhakikisha biashara zao za madawa ya kulevya zinaendelra kupitis TFF.


Mimi kutoka moyoni nimuunga mkono ndugu Jamal Malinzi,

Na kwa uwezo wangu, nitatumia njia zangu zote za siasa ya soka kuhakikisha taifa linampata Jamal Malinzi aka Havelange kuokoa soka letu na viana wetu wanaogeuzwa makontena huku soka likididimia kila uchao,
 
Mmmmh Soka-kandana-mpira wa miguu-sijui futiboli-sijui kabumbu...mmmh hapa Bongo!! NEVER neva,kamwe ! Kwanza tufunge safari kwenda Zambia tukaulize CHIPOLOPOLO walinyakuaje Ubingwa afrika ?...afu Tuende Ethiopia tuwaulize walifikaje fainali za Afrk.Kombe la Dunia? na hatimaye turuke hadi TOGO tuwashawishi watupe muarobaini waliotumia kufika mashindano ya World CUP.... yanini kujifarguwa kulikoni!
 
Jamal ni oppotunist, alikuwa kwenye ngumi, mziki, nk,

Nyamlani ni kibaraka na sio muwajibikaji,

Sasa nyie watu wa system mmeshindwa kutupa kiongozi bora na nyie mnalalamika humu kama sisi? Au mpira hauna issue kwenu maana wanasiasa mmewashindwa!!
 
Jamal ni oppotunist, alikuwa kwenye ngumi, mziki, nk,

Nyamlani ni kibaraka na sio muwajibikaji,
Nimepitia Cv ya Malinzi kwenye mpira nakubaliana na wewe 100%, ameniacha hoi kwenye Trust Fund, wachezaji wanalilia vipato haviwatoshi yeye anataka hata hicho kidogo akifisadi tena..loh.
 
Sasa nyie watu wa system mmeshindwa kutupa kiongozi bora na nyie mnalalamika humu kama sisi? Au mpira hauna issue kwenu maana wanasiasa mmewashindwa!!
Kiongozi bora anatoka katija jamii,

Jamii ikibadilika itazaa kiongozi bora
 
Mi nilifikiri bora huyu kumbe ndo basi kabisa, haki ya nani...Nani wa kuliokoa soka la Tanzania? Kumbe tunarudi enzi za Ndolanga.
 
Nimepitia Cv ya Malinzi kwenye mpira nakubaliana na wewe 100%, ameniacha hoi kwenye Trust Fund, wachezaji wanalilia vipato haviwatoshi yeye anataka hata hicho kidogo akifisadi tena..loh.
Jamali Malinzi ni mwanamichezo, sidhani kama yupo kama usemavyo
 

Tutayafanyaje hayo bila kupata viongozi thabiti kwanza?

Tumsimike kwanza Jamal kisha atuongoze kufanya hayo yote
 
Nimepitia Cv ya Malinzi kwenye mpira nakubaliana na wewe 100%, ameniacha hoi kwenye Trust Fund, wachezaji wanalilia vipato haviwatoshi yeye anataka hata hicho kidogo akifisadi tena..loh.
Soma na uelewe ndugu yangu, kilichozungumziwa hapo ni kuweka misingi ya wachezaji kujichangia kama ilivyo wafanyakazi wengine ambao wana NSSF na PPF, wewe ulitaka nani awachangie? Pia jaribu kuelewa maana ya Trust Fund, wachezaji wetu wastaafu wanapata aibu kwa misaada ya public ambayo ni very embarrassing to them, angalia hio picha ya Jella Mtagwa akipewa hati ya kibanda...
 
Jamal ni oppotunist, alikuwa kwenye ngumi, mziki, nk,

Nyamlani ni kibaraka na sio muwajibikaji,
Nini maana ya opportunist? Na wewe kutumia jina la Jason Bourne ambalo ni jina maarufu inakufanya kuwa opportunist?I don't think so. Hebu jaribu kujibu 'why and how' Malinzi kushiriki katika Ngumi na muziki kunamfanya kuwa opportunist.
 
Na hii ni dhana nzuri sana katika kukuza na kuthamini vipaji vya vijana wetu
 
woote dhaifu ila nyamlani hakuna kitu kabisaaa
 
jamal malinzi oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Wajumbe wasipo mpitisha jamal tutawatndika viboko.

Tatizo soka la bongo lishaingia siasa nausimba na uyanga.badala yakuangalia nani anafaa kuwa kiongozi safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…