Elections 2010 Tanzania Inaongozwa Kichizi kweli

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790


Kifungu cha 17 cha sheria aliyonukuu kinasema hivi:


17.-(1) An agreement reached by the Public Service Joint Staff Council or any matter referred to the Public Service Joint Staff Council by the Service Joint Staff Council for approval in relation to any dispute regarding terms and conditions of service of public servants shall be recorded in writing and signed by the Chairman or any other member nominated on that behalf by the Chairman and be forwarded to the Minister.
(2) On receipt of the agreement the Minister shall accept the agreement.

(3) Where the agreement is accepted by the Minister without modification, it shall ipso facto, be an award.

(4) Where the Minister considers that there is a need for further consideration of the matter, he shall refer it back to the Public Service Joint Staff Council for further negotiation.

(5) Every award made shall be final and binding upon the Government and the public servants to whom the agreement relates for a period of twelve months beginning on the date on which the award was made.

(6) No application to negotiate another agreement relating to any matter that has been covered by the agreement or vary the agreement on a matter which involves or which have the effect of making variation to agreement shall, save with the prior permission of the Minister, be placed upon the agenda or discussed by the Public Service Joint Staff Council unless twelve months have expired.

(7) Every award shall be published by the Minister in the Gazette and shall take effect on the date specified in the agreement..


Sioni ambapo sheria hii inapozuia wafanya kazi kuongelea makubaliano hayo; kifungu hiki kinasema kuwa makubaliano yakishapitishwa basi yanakuwa ni halali kwa kipindi cha miezi 12, na hakuna makubaliano mengine yatakayoruhusiwa katika kipindi hicho. Wafanyakazi wamesema wanataka kuwahoji wagombea kuhusu namna watakavyokabiliana na changamoto zinazowakabili wafanyakazi, hawakusema kuwa wanataka kujadiliana na serikali tena kuhusu mslahi mengine ya wafanya kazi. Je ni kweli wanavunja sheria au ni vitisho tu.



Kama viongozi wetu wanashindwa kweli kutafsiri sheria za nchi na kuzisimamia ipasavyo, badala yake wanazipindisha kusudi ziwanufaishe kadri wanavyotaka, tutakuwa tunatawaliwa kichizi kweli kweli
 
Kichuguu thanks mkuu wangu
Hawa watu wanfikiri mitanzania ni mibwege na haijui hizi sheria. Waonee huruma dola iko ICU
 
Asante kwa kutuwekea hiyo sheria. Haionyeshi wapi palipokatazwa kuzungumziwa makubaliano, serikali inataka kuwaonyesha viongozi wa wafanyakazi kwa mwanga mbaya tu.
 
wasimtishe mtu, serikali ina wasiwasi gani si imesema imeongeza mishahara hewa kwa siri.
 
Sasa ingefaa Mgaya aite waandishi wa habari kuwaeleza uchizi huu wa serikali. Wasikawie -- maana Watanzania Bwana, yaliyosemwa na serikali yanaweza kuwakaa akilini kama ni kweli. Waongo wasion na haya!!!!!!
 
Lakini haya yote si aliyaanzisha Muungwana alipowatukana wafanyakazi na kuzikataa kura zao? sasa wanaweweseka na kujiharibia zaid!
 
Hilo neno inagoozwa ni msamiati mpya wa kiswahili au mie tu nimepitwa na wakati?
 
Hilo neno inagoozwa ni msamiati mpya wa kiswahili au mie tu nimepitwa na wakati?
hata mimi mzee. sijui wameitoa wapi lugha hii

Nilifanya makosa katika heading mara ya kwanza, nilipotaka kufanya masahihisho nikakuta kuwa ukishapost huwezi kusahihisha heading tena; huenda mod atanisadia,
 
hata mimi mzee. sijui wameitoa wapi lugha hii

Kumbe huyu ni mzee wako, ndio maana tabia zenu ziko sawa ; kazi yake kuPM watu kama njia ya kutaka kuwatambua ni nani!! Mlegee na mshindwe na njama zenu za kifisadi, mmestukiwa!!
 
Serekali ya CCM inatia aibu!

They are done...!

Wingu jeusi limewaelemea hawaoni hata hatua moja mbele .... watajimaliza wenyewe!! Vitu gani vya kitoto hivyo wanafanya.. wamekosa uchizi mwingine wa kujaribu ku manage makosa yao? Lakini nafikiri hawaoni kuwa wanamakosa yeyote ... na hivyo ndivyo tunavyotaka waendelee kufikiri kwani ndio upenyo wa CHADEMA kupitia kuelekea ushindi!
 
huo mshahara walioongeza 260k ni makubaliano yapi kama sio rushwa?
 
Viongozi walio madarakani wanadhani bado tuko kwenye kile kipindi cha giza ambapo serikali inaweza kudanganya sheria inasema hivi wakati haisemi hivyo na wananchi wote wakawaamini. Shitindi and the like wamepitwa na wakati.

Vile vile, TUCTA sio ya wafanyakazi wa serikali peke yao. Au Shitindi hajui hivyo?

Mgaya kasema TUCTA itawaomba wagombea kuizungumzia kuhusu mipango yao. Kwa nini Ikulu iogope hivyo? Calm down guys. You panick too easily.
 
Lakini haya yote si aliyaanzisha Muungwana alipowatukana wafanyakazi na kuzikataa kura zao? sasa wanaweweseka na kujiharibia zaid!

Sungura karukaruka lakini mkungu hakufikia. Mwishoni akasema sizitaki mbichi hizi. Hii ndiyo janja ya CCM, lakini kifo cha nyani miti yote huteleza.
 
Shitindi == kituko cha taifa.

Nia na madhumuni ya tabaka tawala ni kutawanya watu wasiwe na sauti moja kwa kutumia mbinu za kijinga kama hizo za kutoa tafsiri potofu ya sheria... wanadhani wataendelea kuenjoy free ride ktk gari la 'Tz gullibility' for life, how wrong they are, wanasahau kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Hivi nyie hamjui kuwa Majambazi CCM na vibaraka wake ni VILAZA?
 
so haya mawazo mazuri ni vema vyama vya siasa vikawa mstari wa mbele kuelimisha ambao hawako hapa jamvini maana once mtu akinukuu kifungu cha sheria mwana nchi mwingine ni rahisi kujua kuwa yu sahihi.
 
Kauli ya Rais Kikwete bado inasimama palepale hata wakiongeza mshahara kwa Wafanyakazi.Salama yake inabidi aombe msamaha hadharani,au awaite tena Wazee wa Dar es salaam na kufuta kauli yake! Imefika wakati sasa Viongozi wawajibike kwa matendo/Kauli zao.Kama Kiongozi wa Nchi aliweza kutoa kauli ya dharau/Jeuri kwa Wafanyakazi inakuwaje kwa wale ndugu zetu Wakulima? ambao kwa kiwango kikubwa ni watu wenye upeo mdogo kwa mambo mengi? Gharama ya dharau ile ni lazima ailipe.
 

....Mkuu ni kweli kabisa...............JK alivunja ile philosophy/slogan ya CCM kuwa Chama Cha Mapinduzi ni chama cha Wakulima na Wafanyakazi na hata kwenye bendera yao zile alama za jembe na nyundo ni kwa makusudi kabisa ya usemi huo..............NOW.........kawakana Wafanyakazi kuwa hahitaji kura zao............suala liko wazi kabisa sasa Chama kina wakati mgumu............nilikuwa mkoa juzi juzi kweli hali ni ngumu kwa CCM............na CHADEMA wanatakiwa ku-maintain pressure..............
 
Kuongeza mishara kipindi kama hiki ..... Its simply a corruption na hao TAKUKURU should work with this!!

Wafanyakazi ...wasidanganyike!!
 
Kuongeza mishara kipindi kama hiki ..... Its simply a corruption na hao TAKUKURU should work with this!!

Wafanyakazi ...wasidanganyike!!

Correct kabisa; juzi nilitoa hadithi moja kutoka kwenye hadithi za Esopo hapa na kusema kuwa kufanya hivi ni sawa kabisa na kujipendekeza na kusema uwongo. Yote hayo mawili ndiyo kiini halisi cha rushwa kama ulivyoiweka ndugu yangu. UBARIKIWE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…