Elections 2010 Tanzania Inaongozwa Kichizi kweli

Elections 2010 Tanzania Inaongozwa Kichizi kweli

Hapa ndipo kazi ya waandishi wahabari kunukuru hivi vifungu siyo kaandika tu sheria na 1 bila kunukuru maana magazeti yangenukuru hii sheria watu tungejua ujinga wa huyu katibu msaidizi.
 
Alama ya bendera ni JEMBE na NYUNDO!

Naona viongozi wengi wa CCM wanasahau kuwa tulikariri ahadi zote za chama cha mapinduzi angalipo tu wadogo na kusema fitna kwetu ni mwiko. Lakini leo hii chama kilekile kinawakana wakulima na wafanyakazi. Huu ni ukaidi uliopinda na kupita kiwango. Ukarimu tulioonesha tukiwa wadogo kukitetea chama umemong'onyolewa na viongozi wa chama mwaka hadi mwaka kutokana na yale tunayojionea katika Taifa letu. Na inafikia mahali JEMBE na NYUNDO vinatumika kumong'onyoa!!
 
Rais ni mtu mkubwa sana, kauli yake sisi tunaiheshimu, yeye ndiye alituambia sisi wafanyakazi kuwa hazitaki kura zetu, na hakuna wakati mwingine wowote ambapo amekanusha kauli hiyo, sasa hawa wakuda wanaokanusha wanamtisha nani? Kauli ya mwungwana bado inasimama, HAZITAKI KURA ZA WAFANYAKAZI. Yeye alisema hata tungegoma kwa miaka minane asingeongeza kitu, hivyo hizo 260,000/- ni za Dr. Slaa, nahuyo ndiye mtu wetu. Dr. Slaa na wanyonge, JK na mafisadi, hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom