Pre GE2025 Tanzania inatarajiwa kuwa na Wapiga Kura 34,746,638 watakaoandikishwa katika Daftari la Wapiga Kura

Pre GE2025 Tanzania inatarajiwa kuwa na Wapiga Kura 34,746,638 watakaoandikishwa katika Daftari la Wapiga Kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-06-12 at 13.47.57_23f31f82.jpg
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari, leo Jumatano Juni 12, 2024 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya majadiliano kuhusu mandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakaoanza Julai 1, 2024.

UBORESHAJI WA DAFTARI
Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya Uchaguzi Mkuu na kabla ya siku ya uteuzi. Wanaohusika katika zoezi hili ni Wananchi ambao: -
  1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
  2. Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025;
  3. Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine;
  4. Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari;
  5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
  6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika.
Watendaji wa Uandikishaji / Uboreshaji
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na:-
  1. Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa;
  2. Maafisa Waandikishaji;
  3. Maafisa Waandikishaji Wasaidizi;
  4. Waandishi Wasaidizi; na
  5. Mwenyesha Kifaa cha Bayometriki
Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura
Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.

Wajibu/Majukumu ya Mawakala wa Uandikishaji
  1. Kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
  2. Kushirikiana na Waandishi Wasaidizi kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio na sifa.
Pamoja na majukumu tajwa, Mawakala wa Uboreshaji hawaruhusiwi kufanya yafuatayo:-
  1. Kuingilia shughuli za uendeshaji wa zoezi la Uboreshaji. Msimamizi wa kituo ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya nani anastahili kuandikishwa au kuboresha taarifa zake kwa mujibu wa Sheria.
  2. Kufanya kampeni za kisiasa katika kituo cha uandikishaji
  3. Kuorodhesha majina ya watu wanaojiandikisha.
Kiapo cha Kutunza Siri cha Mawakala wa Uandikishaji
Kila Wakala wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, ni lazima kula kiapo cha kutunza siri za taarifa za mwombaji au Mpiga Kura aliyeandikishwa. Wakala atakula kiapo mbele ya Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Wakala wa uandikishaji katika kituo cha kuandikisha Wapiga Kura hakuzuii utekelezaji wa majukumu ya Uandikishaji Wapiga Kura.

Watazamaji wa Uandikishaji
Kwa mujibu wa Kanuni za 46, 47, 48, 49, 50 na 51 (1) za Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Watazamaji wa ndani na kimataifa, wanaruhusiwa kutazama mchakato wa Uboreshaji utakavyofanyika katika vituo vya Uandikishaji.

Watazamaji wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutembelea vituo vya Uandikishaji, ni lazima waombe na kupatiwa idhini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Watazamaji. Aidha, Watazamaji 24 watakaoruhusiwa na Tume watapewa barua za kuwatambulisha kwa Maafisa Waandikishaji na Mwongozo wa watazamaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume. Maafisa Waandikishaji watatakiwa kuwapa barua za kuwatambulisha kwa Watendaji wa vituo ambavyo watavitembelea. Aidha, Watazamaji wa Uandikishaji wa Wapiga Kura hawapaswi kutoa maelekezo kwa Mwandishi Msaidizi katika kituo husika.

Kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura
Kwa mujibu wa Kifungu vya 11 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:
  1. Kulikagua Daftari;
  2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
  3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
  4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali
Kifungu cha 27 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura. Kifungu cha 28 Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, kinaweka utaratibu wa kuweka pingamizi. Mtu aliyewekewa pingamizi hutakiwa kupelekewa taarifa ili aweze kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba (7).

Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Mahakama itapaswa kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kupokea rufaa hiyo, uamuzi wa Mahakama ya Wilaya na iwapo aliyewekewa pingamizi hakubaliani na 25 maamuzi ya Afisa Mwandikishaji ya kuendelea kukataliwa kuwemo katika Daftari, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi Wilaya ndiyo utakuwa uamuzi wa mwisho na mtu hatoweza kukata rufaa katika Mahakama nyingine yoyote.

WhatsApp Image 2024-06-12 at 13.47.59_29b67acc.jpg
UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA KUFANYIKA KWA SIKU 7 KILA KITUO
Wakati uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ukitarajiwa kufanyika Mkoani Kigoma, Julai Mosi, 2024 imeelezwa uboreshaji utaanza siku hiyohiyo na kuendelea katika mikoa ya Katavi na Tabora, ikifuatiwa na Kagera na Geita.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima amesema zoezi hilo litaendeshwa kwa siku saba kwenye kila kituo cha kuandikisha Wapiga Kura na wanatarajia Awamu ya Kwanza itakamilika Machi, 2025 kisha Awamu ya pili itafanyika Aprili hadi Juni 2025.

Aidha, amesema mchakato huo una lengo la kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi na kuwa uboreshaji wa Awamu ya Kwanza utafanyika kwenye mizunguko 13.

WhatsApp Image 2024-06-12 at 13.47.52_309616fb.jpg

WhatsApp Image 2024-06-12 at 13.47.55_85826d99.jpg
TAKWIMU ZINAZOTARAJIWA KATIKA MABORESHO YA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Mkurugenzi wa Uchaguzi (Katibu wa Tume), Ramadhani Kailima amesema kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Wapiga Kura 5,586,433 wapya wanatarajiwa kuandikishwa ambao ni sawa na Asilimia 18.7 ya wapiga kura 29,754,699 waliopo kwenye Daftari

Amesema takwimu hizo zimepatikana baada ya uboreshaji uliofanyika Mwaka 2019/20 ambapo Wapiga Kura 4,369,531 wanatarajiwa wataboresha taarifa zao.

Wapiga Kura 594,494 wanatarajiwa wataondolewa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari. Hivyo, baada ya uboreshaji, inatarajiwa kuwa Daftari litakuwa na jumla ya wapiga kura 34,746,638.

Aidha, idadi hii inaweza kuongezeka ikiwa kutakuwa na waliokwama kujiandikisha Mwaka 2019/20 licha ya kuwa na sifa.


Idadi ya Vituo vya Kuandikisha Wapiga Kura
Vituo 40,126 vya kuandikisha Wapiga Kura vitatumika katika Uboreshaji wa Daftari 2024, kati ya hivyo Vituo 39,709 vipo Tanzania Bara na 417 vipo Zanzibar.

Hili ni ongezeko la Vituo 2,312 ikilinganishwa na Vituo 37,814 vilivyotumika Mwaka 2019/2020.
 
Kupiga kura chini ya tume na mazingira haya ni matumizi mabaya ya raslimali muda. Wenye muda wa kupoteza tu au wanaofaidika na huo uhuni uitwao uchaguzi ndio watashiriki.
 
Ccm weka mazingira sahihi yaliyo huru na wazi katika uchaguzi, hizi sheria zilizowekwa na serikali yenu kamwe hazitoi haki ya kuchaguliwa mtu aliye nje ya ccm! Hofu yenu kutoka madarakani inaligharimu taifa acheni udikteita!
 
Back
Top Bottom