Tanzania inavyoweza kupiga Hatua Kiuchumi na kielimu

Tanzania inavyoweza kupiga Hatua Kiuchumi na kielimu

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
6,559
Reaction score
12,518
So far hapa tulipofika kuna watu wamepambana lakini haiondoi ukweli kuwa bado tupo nyuma. Huu ndio ukweli wa wazi
Nimekuwa nikiwaza kwa namna gani tunaweza kupiga hatua mawazo yangu yakanituma kutazama vilabu viwili Simba na Yanga ambavyo vimepiga hatua walau nakutuweka kwenye ramani ya nchi za mpira afrika.
Mafanikio haya pamoja na jitihada binafsi za wazawa ambazo kimsingi hazipaswi kupuuzwa lakini mtu yeyote mwenye akili Timamu atakubaliana nami kuwa "MAFANIKIO YA CLAB HIZI MBILI YAMECHAGIZWA KWA KIASI KIKUBWA NA WAGENI" (wachezaji na viongozi)

WAGENI , ndio hoja ya msingi katika andiko hili, niwakati sasa wakuwa na wataalamu wa kigeni katika mashirika yetu, na taasisi zetu, Taasisi za elimu kama vyuo na kadhalika niwazi kuwa tunahitaji watenda kazi wa kigeni zaidi ili kututoa hapa tulipo. Tusione haya ila tunaweza kutumia nafasi hiyo kujifunza zaidi. Tunaweza kuunda idara nyeti za kusaka wataalamu wa kigeni kote duniani kwaajili ya kuja kuboost. Pamoja na kuwa nigharama lakini nadhani inaweza kututoa hapa tulipo. Badala ya kun'gang'ania wataalamu wa ndani ambao kimsingi mpaka sasa tulitakiwa kuwa mbali zaidi. Niwakati sasa wataalamu wa ndani wapigane kushindana na wataalam wa kimataifa hii itachochea utendaji . Jambo hili linahitaji roho ngumu na moyo wa ujasiri unaolenga tija kuliko kumrithisha mtu mmoja mmoja

"Tunahitaji wageni kutusukuma tutoke hapa tulipo huku tukijifunza kutoka kwao, niwakati sasa wataalamu wa ndani washindane kiutendaji na wataalamu wa kimataifa" mimi mstahiki mea yangu ni hayo tu
 
Wewe unaonaje mkuu au utasema nikuweka rehani ajira zetu😃🤣
 
Huu ndo ukweli hata kina north Korea walifanya hihivi pia , Sasa tatizo ni mtazamo wa kitanzania gususani watawala , wanao amini kilakitu ni mtanzania kwanza mambo mgumi hayawezi tatuliwa na akili ndogo ni Bora tutafute akili kubwa zipandikize maarifa
 
Shida sio uwezo wa watanzania ndugu, tatizo ni culture ya upigaji na ufanyaji mambo serikalini.

Wenyewe hawataki hiyo culture ibadilike, kuna diaspora wataalamu washajaribu kurudi ohoo wanataka kusaidia nchi na wakapata kazi serikalini.

Baada ya miaka 2 on avarage, wenyewe wanafungasha virago na kurudi hizo nchi walizokuwa wanaishi.

Usifanye mchezo, yaani we uende na taratibu zako za sijui namna ya kufanya mambo kwa cost efficiency za mradi, sijui tender za mikoani umpe most qualified person (wakati wenzako wanauza kwa mwenye dau kubwa au kutoa kwa kampuni zao).

Ndugu huko serikalini kuna culture ya ajabu ni ngumu sana kwa mtu mwenye nią ya maendeleo kufanikiwa.

Ushajiuliza kwanini Dorothy Gwajima alitolewa afya au Jerry Slaa ardhi?
 
Tuuondoe ushirikina kwanza ndio tutaenda mbali
Screenshot_20250627-104131.jpg
 
Sawa uko sahihi! Angalia Mauritius nusu wahindi robo Waafrica na robo wazungu! Pia angalia Singapore nus Wachina nusu Malay! Haya mataifa yameendelea sana! Sisi tunawagopa wageni eti watachulua kazi za wazawa! Hata hapa Tz angalia aliko Mchaga pameendelea! TUSIWAOGOPE WAgENI WATATUPA MWANGA WA MAENDELEO
 
Back
Top Bottom