Ndugu zangu hii nchi yetu haitakiwi iwe hivi ilivyo sasa. Kuna Watanzania wengi wajanja na wabunifu na Mungu katupa mengi.
Sasa inashangaza kama wananchi tunakubali tu mambo ya ajabu ajabu yaendelee nchini kama vile hayatuhusu. Tuache kwa mara moja kufikira sisasa na kufikiria nchi.
Mfano katiba nzuri sio swala la kichama ni swala la kitaifa. Mikataba sio swala la kichama ni swala la kitaifa. Uzalishaji ni swala la kitaifa. Kodi na mapato ni swala la kitaifa.
Mifumo ya elimu na Afya ni maswala ya kitaifa. Rushwa ni swala la kitaifa. Sasa ni kwanini haya maswala ya kitaifa hayashughulikiwi na sisi wenyewe hatuonyeshi uchungu wa nchi yetu. Sheria ni swala la kitaifa.
Tusije kusubiria upinzani au wengine watuonee huruma.
Lakini tusifikirie kisiasa kila kitu bado kunaweza kuwa na ushindani na maendeleo pamoja.
Kama jamii huwezi kuruhusu rushwa na kuichekea na kusubiri maendeleo! tunaona wagombea wa upinzani wanakatwa tujiulize kama hatutaki demokrasia ni kwanini tusiwe na mfumo mwingine badala ya serikali kutumia mabilioni kwenye chaguzi feki na watoto hawana shule.
Kama ushindani kwenye siasa ni mfumo mzuri basi tuamue sio kuwa nusunusu.