Masaka... sikujua unaguswa na matatizo ya Tanzania. Ulipojitokeza kutetea CCM miye nilikuwa nahesabu muda tu kabla "mwanga wa ukweli" haujakuzukia. Inasikitisha kuona CCM inapoteza mtetezi mzuri kama wewe. Nina uhakika watakumiss.
Ila nakuomba usikate tamaa, jaribu kutetea unayoweza kwani mchango wako ni muhimu sana na ulileta balance ya pekee humu. Chonde chonde usiache kukitetea chama chako.
Usikate tamaa mapema namna hiyo.. Bado una nafasi kubwa ya kukikosoa chama chako ukiwa ndani ya chama hicho
naona hizo video zimeondolewa zote ktk youtube....au...
Sasa wale wasafi walijifunza usafi kutoka kwa nani? Na wale waishio kwenye mwanga nani aliwatoa gizani?
Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi, kufuatilia comments za watu nikakuta link kwenda youtube kuona documentary kuhusu maisha ya uwanja wa fisi - inaitwa hyena square.
Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Inaumiza kuwa wengine tunaishi maisha ya kula na kusaza huku wenzetu wakipitia maisha kama ya dada Eliza aliyotajwa kwenye hiyo movie.
Kama haya yanatokea Tanzania na mimi sikuyajua, sijui ni mengi kiasi gani ambayo siyajui. Hapana, hii imepita kipimo, kama hii haivunji moyo basi sijui nini tena kitabadili mwelekeo. Siwezi sasa kuendelea kuishi maisha mazuri wakati wengine wakiishi jehanam kama haya. Kama haya yanatokea Tandale ambako ni KM chache tu toka magogoni, sijui yanayotokea Iringa ni makubwa kiasi gani.
Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.
Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.
Hebu one mwenyewe hii clip ya youtube..
[media]http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM[/media]
[media]http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc[/media]
Masaka, kama alivyouliza KKN, ulikuwa hujui matatizo ya Tanzania, au ulikuwa unatetea CCM kama mimi ninavyotetea Pan Africa, au uliyajua matatizo lakini hukujua mengine yanasababishwa na uongozi mbovu wa Sisi em, au ulikuwa unatetea maslahi fulani, au, ulikuwa unataka kuleta changamoto jamvini tu?
Sidhani kama clip ya dakika 20 ya Uwanja wa Fisi, ambayo hata haitoshi kuanza kueleza matatizo ya Tanzania, ikawa ndio epiphany kwako.
Nisaidie kuelewa kwa nini nisiseme ulikuwa una feki mawazo yako, una intellectual dishonesty.
Ahsante.
Kama huzipati Youtube basi unaweza kuzipata EastAfricanTube kupitia http://www.eastafricantube.com/media/9686/JITAMBUE_PT.1/ and http://www.eastafricantube.com/media/9683/JITAMBUE_PT.2/
Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi, kufuatilia comments za watu nikakuta link kwenda youtube kuona documentary kuhusu maisha ya uwanja wa fisi - inaitwa hyena square.
Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Inaumiza kuwa wengine tunaishi maisha ya kula na kusaza huku wenzetu wakipitia maisha kama ya dada Eliza aliyotajwa kwenye hiyo movie.
Kama haya yanatokea Tanzania na mimi sikuyajua, sijui ni mengi kiasi gani ambayo siyajui. Hapana, hii imepita kipimo, kama hii haivunji moyo basi sijui nini tena kitabadili mwelekeo. Siwezi sasa kuendelea kuishi maisha mazuri wakati wengine wakiishi jehanam kama haya. Kama haya yanatokea Tandale ambako ni KM chache tu toka magogoni, sijui yanayotokea Iringa ni makubwa kiasi gani.
Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.
Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.
Hebu one mwenyewe hii clip ya youtube..
[media]http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM[/media]
[media]http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc[/media]
Endelea na ubishi wako wa kisomi ambao mpaka leo hii na mimi nilikuwa naufanya bila kugundua kuwa ubishi wa kisomi hauleti suluhisho lolote la matatizo. Kwa ubishi huu unaotaka kuuanzisha labda kwa nia ya kubadili mwelekeo wa thread hii, jua kuwa utabishana na wengine lakini sio mimi.
Asante.