Mwaka 2006 nilitembelea BONGO wakati mambo ikiwa mbaya sana kwa wananchi kwa ajili ya UKAME NA UMEME ULIOSHINIKIZWA NA UJAMBAZI WA RICHOMD.
Nilipokuwa kwenye mizunguko yangu kwenye jiji la Dar kuonana na watu wangu nilimpa ride tu maeneo flani na pembeni kulikuwa na saloon a kina dada ambao walikuw wamekaa nje kwasababu hakuna biashara na hata air condition haifanyi kazi na kafeni kenyewe kaliko ndani kanapuliza joto badala ya hewa nzuri.
Ghafla akatokezea CHINGA MMOJA ambaye alikuwa amepigika kinoma huku malapa aliyovaa yakiwa hovyo hovyo huku kisigina kikiwa kinakanyaga chini!
Hutu chinga likuwa akiuza vyupi na sidiria akiwa amekamata mkononi huku akimlilia dada mwenye saloon anunue walau sidiria moja ili aweze kwenda kula!
Mjadala uliendelea huku chinga akiongea hadi mapovu meupe yakimtoka pembezoni mwa mdomo na huku akionekana kuwa maisha ni magumu na hata hali yake kiafya ni mbovu kutokana na mlo wa kubabiababia!
Mimi kuwa kwamngu pembeni kulinipa shida kwani nilkuwa sijui nimtetee yupi!
Chinga anasema hajala na anategemea kina dada wananunue sidiria ili walau akale...
Mwanadada wa saluni naye akawa nadai hata yeye anafunga muda si mrefu ili akajaribu kuangalia kama nyumbani kuna chakula kwani hajafanya biashata kwa karibu wiki kwasababu ya umeme.
Mabishano yalikuwa makali...Lakini wote waalikuwa hawana makosa...UCHUMI WETU ULIKUWA UMELALA EXCEPT KWA MAFISADI MAFIOSO ambao wao mambo ni mswano tu na migenerator huku wakiendelea kulipwa pesa za wananchi kwasababu tu RICHMOND ilishindwa ku provide umeme wa dharura kwa wananchi na hivyo mabilioni yao ya kodi kupewa kina ROSTAM,MKAPA,KIKWETE,LOWASSA,MRAMBA,MGONJA NA MAFIOSO WENGINE WA CCM!
Dada wa Saluni naye alikuwa akihitaji sidiria lakini hana pesa...Chinga akaomba walau mia saba ili akale...Dada akawa still hana...Na chinga kaanza kuchukia akidhani kuwa Dasa ni tajiri mwenye roho mbaya!
Nikatoa elfu nikampa nikamwambia ampe Dada hiyo sidiria...
Nikachoma gari moto huku machozi akinitoka!
EMPATHY TUME LACK...Afadhali sasa wengine nao wamegundua na kulia baada ya Kelly.
.....short & powerfull story how society inavyosuffer kutokana na ulafi wa mafisadi,mzee umegusa point zote jinsi rushwa ilivyoua biashara ya huyo dada na kuondoa purchasing power yake na kusababisha machinga alale njaa indirect kutokana na rushwa za kina lowassa na wenzake...na huo ni mfano mmoja tuu,millions wako affected na hizi tabia za mafisadi,nina uhakika kuna waliouwawa kwa kufanya ukibaka ili wale kutokana na njaa.