Tanzania Internationaly, Young Africans & Azam FC

youngsharo

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
2,491
Reaction score
500
Tanzania ikiwa inaangaliwa kimataifa kupitia timu zake za vilabu kwenye mashindano ya klabu bingwa na shirikisho, tayari Yanga Na Azam wanajiandaa na michezo yao ya raundi ya kwanza itakayochezwa mwishoni mwa wiki,
Kiujumla Timu hizi bado zipo katika perfomance nzuri, ukiziangalia katika msimamo wa ligi ndizo timu zinazoongoza Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na Azam wakiwa nyuma kwa nafasi moja, kwa maana ya kwamba wapo nafasi ya pili kwenye ligi.

Tatito linakuja kwamba katika miaka yote au kihistoria timu za Tanzania zimekuwa hazifanyi vizuri kimataifa zaidi ya kuishia kwenye hatua ya mtoano jambo ambalo uongozi wa soka la Tanzania umeshindwa kulipatia ufumbuzi.

mashindano ya mwaka huu kwa upande wangu natupa jicho zaidi kwa Azam ambaye atakaa kuiwakilisha Tanzania kama "Bingwa" tofauti na tulivyozoea akiwa anaiwakilisha kwenye shirikisho.

Upande wa Yanga si sisemi lolote, coz siiamini sana labda tu kudra za mwenyezi mungu ndo zinahitajika.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,

MUNGU IBARIKI YANGA,

MUNGU IBARIKI AZAM.
 

Naona leo umeamua kwenda na uhalisia na sio kihisia, hata hivyo bahati mbaya kwa Azam anaweza akajikuta anaishia hatua hii hii ya kwanza kutokana na timu aliyopangiwa. Yanga unaweza ukaona hawako vizuri sana lakini wanaweza kukushangaza, kwa timu waliyopangiwa wanaweza kuendelea hatua inayofuata. Kuna watu kama huyo mliberia, Niyonzima, Mbuyu Twite, Ngasa, Msuva na Nadir kocha akiwatraini vizuri wanaweza kuwafikisha mbali bila kusahau uzoefu wa Dan Mrwanda na Tambwe akipata mtu mzuri wa kumshauri na kumwondolea anachowaza kwa sasa bado naye ni mzuri.

Mwisho kabisa nawatakia kila la heri Azam na Yanga lakini hata wakitolewa mapema poa tu maana uwezo wao ndo utakuwa umeishia hapo.
 

Kwa Azam kuishia hatua hii ya awali haitashangaza, lakini kwa Yanga kuishia hatua hii itakuwa ni fedheha kubwa.
 

tusubiri tu tuone.
 
Mwaka huu Yanga lazima ifike fainali ya Kombe la Shirikisho na kubeba ubingwa huo kwa mara ya kwanza ili mikia wakae kimya kabisa.
Mkuu unajitafutia matatizo bure, pale hamna timu ya kufika hata hatua ya makundi sana sana mkijitahidi sana (ambako sijui kama mtafika) mnaweza kufika ile hatua ya jamaa wanaoshindwa ligi ya mabingwa na kuletwa kombe la shirikisho na ndo watakaokuja kuwaondoa, kwenye hilo kapu waarabu na timu za africa magharibi hazikosekani.
 

Mtoano siyo sawa na ligi kama ile ya Super 8 ya Klabu Bingwa, watatoana wao kwa wao, sisi tutakayekutana naye, itakula kwake! Si unakumbuka ninyi mlivyofika fainali kimiujiza (Kama kuna timu nimesahau I stand to be corrected):

1. Mliwatoa Ferroviario ya Msumbuji kwa faida ya bao la ugenini baaada ya kutoka suluhu Dar na sare ya 1-1 huko Msumbiji,
2. Mliwatoa Atletico Aviacao ya Angola (ndugu moja na LIBOLO FC ),
3. Mliwatoa El Harrach ya Algeria,
4. Mkatolewa na Stella Abidjan fainali; baada ya Boli Zozoo kuwalamba chenga mabeki Rashid Abdallah na Kasongo Athman mara mbili.

Si umeona jinsi mlivyotinga fainali kiurahisi! Hakuna cha Misri wala Tunisia.
 

we hizo timu nyingine usizitaje bwana unawakumbusha watu machungu. [LIBOLO]
 

Waarabu2 hata waje kanjibhai.
 
Mkuu sikutegemea hoja nyepesi kama hii kutoka kwako. Nilidhani wewe utakuwa ni mtu unayejua michuano ya mtoano inavyokwenda. Nimekushusha rank kidogo.
Kwa mtu anayefahamu muundo wa mtoano, kama ukiona Misri na Tunisia hawajapita mkondo wako, basi ujue kuna wababe wao waliowatoa ndio unaokutana nao. Kwa lugha hii, kikwazo cha Yanga kufika walau nusu fainali huwa ni Misri na Tunisia! Umesahau 6-0 za Raja Casablanca ya Morocco?
 

Awali ya yote Mkuu Jabulani sihitaji kuwa ranked na wewe kwani huna ufahamu huo. Pili hao unaowataja tayari nimekujibu niliposema watatoana wao kwa wao halafu atakayepenya hapo akikutana nasi itakula kwake, hebu rudia kusoma post yangu. Hizo bao 6 zilikuwa katika mtoano? Nakukumbusha: zilikuwa katika Super League ambayo tayari nimeizungumzia katika post yangu.

Natambua Mkuu machungu uliyonayo moyoni baada ya timu yako kuendelea kuboronga huku ikiwa haina matumaini ya kupata hata angalau nafasi ya uwakilishi kimataifa.

Nilitegemea ungenipongeza kwanza kwa kumbukumbu nzuri niliyoiandika kwa manufaa ya kizazi hiki maana si wote walikuwepo miaka 22 iliyopita.

Nimekumbushia timu zilizocheza na Simba kwa mpangilio, nimetaja hadi mabeki wa Simba mwaka ule na hata mfungaji wa mabao yote ya mabingwa, ulitaka niseme nini zaidi? Au ulitaka niandike: 'Kama si hujuma za Dewji, Simba ingechukua ubingwa'? Ujinga ambao wanasimba wamekuwa wakiaminishwa!
 
Last edited by a moderator:
Makoye Matale usiumize kichwa, wengine wapo jf kwa ajili ya kubishana tu, hata kama anaelewa lakini bado anakuwa mbishi.
 
Last edited by a moderator:
Makoye Matale usiumize kichwa, wengine wapo jf kwa ajili ya kubishana tu, hata kama anaelewa lakini bado anakuwa mbishi.

Wamevurugwa vibaya na matokeo ya timu yao hata ufahamu umewatoka, pole zao, acha wajifunze hasara za kushabikia timu zisizo za maana.
 
Last edited by a moderator:
Wamevurugwa vibaya na matokeo ya timu yao hata ufahamu umewatoka, pole zao, acha wajifunze hasara za kushabikia timu zisizo za maana.

lakini mi niwashauri ushabiki wa mpira sio kama uumini wa dini, wahame tu Simba
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…