Tanzania ipo kwenye balehe...

Tanzania ipo kwenye balehe...

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Nchi yaweza kuchukuliwa kama kiumbe ambacho kina baathi ya sifa ambazo mwanadamu anazo na sifa ambazo haiwezi kuzipata kutokana limitation ya kwamba nchi inaexist katika mind construct ( shared belief) kwamba watu ambao wapo ndani ya mipaka ambayo inaweza kuwa physical au imaginary line drawn kutenganisha pande za nchi mbili.

Sasa basi kwa sababu nchi imeumbwa kutokana na idea iliotoka kwenye mbongo ya binadamu hali hii hufanya nchi kuwa na tabia kama za binadamu kwa sababu imeumbwa na binadamu, imezaliwa na ubongo wa binadamu.

Pia nchi huwa na umri na mda tangia watu wakubaliane kwamba kuanzia sasa tupo ndani ya nchi moja inatofautiana baina ya mataifa. kwa mataifa ya afrika mengi ni machanga kwani yamepata uhuru miaka ya sitini lakini kuna mataifa ya ulaya yana karne na karne kujitambua kama ni mataifa.

Bado hakuna anayejua juu ya mda ambapo taifa litachukua mda kukomaa kifrika kwani siku zote mataifa yanaendelea kukua. mataifa ukuaji wake kama wa watoto endapo taifa likiwa changa litaanza na sera ambazo hazina mashiko ( sera ambazo haziwezi kufanya kazi ) basi taifa hilli litaendele kuwa changamoto kila kukicha kutokana na kuwa na misingi ambayo sio imara.

Natoa mifano ifuatayo ili ambao hawajaelewa nazungumza nini waweze kuelewa. amerika ni taifa lilipata uhuru miaka ya 1776 na misingi ambayo serikali iliweka ni kwamba majukumu makuu ya serikali ni kuhakisha kwamba kila mwananchi wake ana uhuru wa kufanya mambo yake billa kuingiliwa na nyombo vya serikali kama hayo mambo hayazuru mtu yeyote, pia msingi mwingine ni kutenganisha serikali na kanisa kwamba nchi haina imani bali watu wake ndo wana imani , kwa hiyo serikali haitahangaika na imani za watu kila mtu ana uhuru wa kuamini kile atakacho. kwa mataifa ya mfumo wa demokrasia amerika ndio taifa kongwe ambolo limekomaa kulinganisha na nchi nyingine na bado lina baadhi ya shida hapa na pale tunaziona.

Sasa turudi kwetu tanzania kwa kuangalia bado ni taifa changa sana ni miaka hamsini tu maana kuna watu wapo kabla nchi haijapata uhuru mpaka sasa wapo. kwa kusema ipo kwenye balehe ni kutokana na mihemuko na matamko yatolewayo kila kukicha kama mtoto ambaye yupo kwenye balehe anajifunza kufanya maamuzi yake mwenyewe.

Sifa za mtoto mwerevu akiwa kwenye balee anatakiwa kujua kwamba bado mbongo yake haijokomaa kumwezesha kungamua varible ambazo zita affect matendo atakayofanya hivyo basi kuwer mnyekekevu kwa wakubwa wake ambao anaona wapo kwenye same page ( kuna baadhi ya watu ni wakubwa kiumri lakini ni akili ni watoto ) hivyo anakuwa makini na kujiahakikishia mkubwa naye mfwata ni mkubwa na ana malengo na mimi kufanikiwa ( sio kila mkubwa anataka mdogo akuwe ajitegemee kuna wakubwa hawependi kuona mtu anakuwa na kuanza kujitegemea hivyo kukosa heshima na unyenyekevu wanaoutaka).

Nadhani kwa watu wadhima kwa tabia hili taifa letu linavyoonyesha kwa sasa ya kurukia kila jambo inaonyesha ni jinsi gani tuna tafuta anguko tusipo kaa chonjoo. na kuja kujutia baadae mda tuliopoteza wa kufanya mambo ya maana. huku kujifanya twajua kutenda ni kicheko kwa mataifa ambayo yamekomaa ( haya mataifa yatakuwa yanashaanga kama watu hawawezi kujisimamia wenyewe watawezaje kujitawala)

So ndugu zangu wacha niendelee kuona watu wanavyo jifurahisha na kujitekenya na kucheka wenyeewe. na napenda kutoa rai kwa wanaozani wanatuongoza kwamba wangalie jinsi history itakavyokuja kuongelewa juu yao. Jinsi gani walivyokuwa wapumbavu au jinsi gani walivyokuwa na uthubutu wa kutembea kwenye kingo juu ya mlima mrefu ili kuona nje ya ukungu uliotanda.
 
Kidogo una matatizo ya ki uandishi. Huna Kona, nukta wala herufi kubwa. Lakini fasihi yako imesomeka.
 
Wachache watakuelewa ...kimombo hiki ndo kipindi cha foolish age, kila kitu kwao ni valuable
 
Back
Top Bottom