Tanzania ipo tayari kuilisha Dunia

Tanzania ipo tayari kuilisha Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
IMG-20230317-WA0010.jpg

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Benki ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Kilimo, Tanzania imeongeza mauzo ya nje ya chakula mwaka hadi mwaka, huku chakula hicho kikiuzwa nchi za Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Pembe ya Afrika (Horn of Africa) na sehemu nyingine mbalimbali duniani.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania iliucha mboga mboga zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.01 (Shilingi trilioni 2.4) katika kipindi cha miaka mitano kati ya mwaka 2018 hadi 2022.

Tanzania pia iliuza mazao ya nafaka (zaidi mchele na mahindi) yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 999 (Shilingi trilioni 2.3) katika kipindi hicho cha miaka mitano iliyopita.

Mauzo ya nje ya nchi ya samaki na bidhaa za samaki yalifikia Dola za Marekani milioni 800 (Shilingi trilioni 1.9), wakati matunda yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 71.4 (Shilingi Bilioni 170) kati ya 2018 na 2022.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa watano wa mchele kwenye bara zima la Afrika na ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa mchele Afrika Mashariki.

Katika msimu wa 2020/21, Tanzania ilizalisha tani milioni 1.85 za mchele, wakati mahitaji ya nchi kwa mwaka ni takribani tani milioni 1. Maana yake ni kuwa mchele wa ziada ulikua tani 850,000.

Katika msimu huo huo, Tanzania ilizalisha tani milioni 6.5 za mahindi, ukilinganisha na nahitaji ya taifa ya tani milioni 6 kwa mwaka.

Takwimu hizi zinaibuka huku Rais Samia Suluhu Hassan leo akizindua maandalizi ya mkutano mkubwa wa Kilimo wa Afrika (Africa Food Systems Forum) ambao unatarajiwa kufanyika Tanzania Septemba 5-8, mwaka huu.

Uzinduzi huo umefanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Tangu aingie madarakani mwezi Machi 2021, Rais Samia ameongeza bajeti ya serikali kwenye kilimo maradufu kwa viwango ambavyo havijawahi kuonekana tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Serikali ya Samia imewekeza kwenye ruzuku ya mgbegu, ruzuku ya mbolea, uzalishaji mbegu na kilimo cha umwagiliaji.
 
Ukichukulia takwimu za miaka jumuishi utaona ni fedha nyingi ila ukichukua mwaka 1 unaona kabisa hakuna tufanyalo, tunazidiwa na Ukraine iliyo vitani inaingizi pesa nyingi kuliko sisi.

Matunda yameuzwa kidogo sana
 
Hizo taakwimu hazipendezi kabisa ukilinganisha the potential. Nchi zingine kama Congo hubarikiwa na kila kitu isipokuwa amani. Tanzania imebarikiwa namna hiyo tu na zaidi yake mkapewa amani lakini hizo taakwimu ziko chini sana tuseme ukweli ....hapo kwa samaki ndio kidogo panapendeza tu....nimejaribu kuelewa sababu lakini sijaweza hadi kwa sasa.
Yaani Tanzania has less than $5M in Beef exports
Yet Tanzania has one of the largest agricultural arable land in Africa na karibu yote ni rain-fed sasa bado irrigation which would probably double the current figures alafu tena the land is probably the cheapest in Africa.

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo kubwa tulilolkuwa nalo hivi sasa Watanzania ni matumizi mabaya ya takwimu, na baya zaidi zinapotumika katika kiki za kisiasa. Ongezeko la mauzo ya nje ni jambo la kujivunia kama nchi kiuchumi, kwani huakisi " competitive & comparative advantages" tulizokuwanazo.

Lakini, nyuma ya takwimu hizi huku nyingine nyingi zikiwa za kupikwa haziendani kabisa na afya nzuri ya uchumi wa jumla ama uchumi wa mtu mmoja mmoja, yaani "aggregate or individual economy".

Hivi kweli unaweza kumshawishi mkulima wa mpumga wa Mbalali ama Madibira kuhusu takwimu za matrilioni ya shilingi yaliyopatikana kutokana usafirishaji wa mchele nje ya nchi na akakuelewa kweli! Kwa Bakhresa ni sawa, kwa kuwa ni sehemu ambayo kampuni yake tanzu ya AZAM inaneemeka.

Jambo lingine la kuogofya, ni matumizi ya takwimu hizi yaliaanza kutumika kama kiki ya kisiasa wakati wa utawala uliopita wa JPM, lakini naona hata huu wa sasa nao unaanza kujikita sana hapa.

Matumizi ya takwimu ni muhimu, ila ni muhimu pia yaendane na ubora wa bidhaa na huduma zilizopo sokoni. Ni jambo lisiloingia vyema akili kwa kutafuta kiki kupitia upande wa sifa za wingi wa vitu, yaani "quantitative traits" na huku tukikwepa kwa makusudi kuangalia uhalisia wa sifa ziendanazo na ubora wa vitu hivyo, yaani "qualitative traits".
 
Jambo lingine la kuogofya, ni matumizi ya takwimu hizi yaliaanza kutumika kama kiki ya kisiasa wakati wa utawala uliopita wa JPM, lakini naona hata huu wa sasa nao unaanza kujikita sana hapa.
Toka mwanzo ulikuwa na points nzuri kuhusu huu mjadala mpaka ulipochomekea hiyo point tu ndipo ukaharibu kila kitu. Inasikitisha sana pale wasomi wetu mnapokuwa watumwa wa siasa uchwara kiasi kwamba mtu unakuwa uko tayari ku-sacrifice usomi wako kwa lengo la kukidhi matamanio ya kisiasa. Too bad 👎
 
Waziri wa Kilimo anaipeleka wizara hii kisomi zaidi, anajitahidi mpaka kutoa takwimu. Sio hao mawaziri mizigo wengine!
 
View attachment 2555507
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Benki ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Kilimo, Tanzania imeongeza mauzo ya nje ya chakula mwaka hadi mwaka, huku chakula hicho kikiuzwa nchi za Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Pembe ya Afrika (Horn of Africa) na sehemu nyingine mbalimbali duniani.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania iliucha mboga mboga zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.01 (Shilingi trilioni 2.4) katika kipindi cha miaka mitano kati ya mwaka 2018 hadi 2022.

Tanzania pia iliuza mazao ya nafaka (zaidi mchele na mahindi) yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 999 (Shilingi trilioni 2.3) katika kipindi hicho cha miaka mitano iliyopita.

Mauzo ya nje ya nchi ya samaki na bidhaa za samaki yalifikia Dola za Marekani milioni 800 (Shilingi trilioni 1.9), wakati matunda yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 71.4 (Shilingi Bilioni 170) kati ya 2018 na 2022.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa watano wa mchele kwenye bara zima la Afrika na ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa mchele Afrika Mashariki.

Katika msimu wa 2020/21, Tanzania ilizalisha tani milioni 1.85 za mchele, wakati mahitaji ya nchi kwa mwaka ni takribani tani milioni 1. Maana yake ni kuwa mchele wa ziada ulikua tani 850,000.

Katika msimu huo huo, Tanzania ilizalisha tani milioni 6.5 za mahindi, ukilinganisha na nahitaji ya taifa ya tani milioni 6 kwa mwaka.

Takwimu hizi zinaibuka huku Rais Samia Suluhu Hassan leo akizindua maandalizi ya mkutano mkubwa wa Kilimo wa Afrika (Africa Food Systems Forum) ambao unatarajiwa kufanyika Tanzania Septemba 5-8, mwaka huu.

Uzinduzi huo umefanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Tangu aingie madarakani mwezi Machi 2021, Rais Samia ameongeza bajeti ya serikali kwenye kilimo maradufu kwa viwango ambavyo havijawahi kuonekana tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Serikali ya Samia imewekeza kwenye ruzuku ya mgbegu, ruzuku ya mbolea, uzalishaji mbegu na kilimo cha umwagiliaji.
Takwimu za kupika, wauzaji wakubwa wa nafaka ikiwrmo mchele huku mnaagiza mchele toka thailand, hebu mfikirie kwa vichwa basi.jpm fufuka uje utuokoe
 
Back
Top Bottom