Kuna ukweli wa wazi katika report hii. Uwezo wa kureason,argue kwa facts na data kwa zama zetu unazidi kupungua sana. Mimi naisapoti report hii kwa experience yangu binafsi katika field hii ya elimu. Miaka ya nyuma tulipokuwa shule Debate zilikuwa za kisomi na nzuri sana. Kama mwalimu/mwanafunzi huchoki kusikiliza kwani watu wanajenga hoja, wanacritisize palepale tena kwahoja nzuri sana lakini kizazi hiki cha kuanzia mwaka wa 2005 kuna mbele ni tofauti na kinatia kinyaa. Si wanafunzi wa secondary au vyuoni ukiwasikiliza mijadala yao utashangaa sana na kupatwa na maswali mengi sana. Ukija kupima pia uwezo wa wanafunzi wetu wa kufaulu,kujituma katika kusoma kwa uvivu na mambo mengine kwa ngazi zote vyuo vikuu mpaka chini utakubaliana na report hii. Kuna mifano mingi sana lakini hawa viongozi wetu wa siasa pia wanaweza kuwa sample nzuri. Nisichokikubali katika report hii ni jinsi wanavyoresearch yao na mfumo wa hizo test. Kwanza sijui ni kina nani wamewafanyia interview na pia katika hiyo interview wamewahoji relevant questions au ndio zilezile waliset huko Amerika? Ukipitia syllabus ya elimu ya CAMBRIGE ukaona mode of assessment na pia mambo wanayoyasoma tena ukafananisha na mfumo wetu wa elimu unaomlimbikizia mwanafunzi mizigo mingi ya masomo hapo pia unapata picha vipi inaathiri IQ yake. Mwanafunzi anaespecialize katika masomo mawili au matatu from the bottom mpaka anapohitimu elimu yake ya juu ni ufahamu wake katika field yake lazima utakuwa mzuri sana kuliko anaebebeshwa masomo kumi O level, manne au matano Advanced level na mawili au moja katika specialization yake jumlisha na mengine matato/matano ya jumla university. Kwahali hii lazima kuwepo tofauti.