Mie kwenye siasa tutakuwa wote ila hili la mpira la leo usiwaseme wale vjana pia nahisi wewe ungekuwa tunakutana tuu kwenye siasa huku kwenye mpira wala ukujui ila kwakuwa watz kila kitu tunajua ngoja nikupe faida, wale algeria wanamlipa kocha ela kibao na timu nzima wanacheza ulaya wako kwao na bado wanaonga na refaree kabla ya dk ya 15 wachezaji wa 3 mabeki wote wana kadi za njano.
Na dk ya 30 anapewa mchezaji wetu red kadi katika mazingira yale hakuna hata kadi ya halali hata moja zote za kuonewa bado wanapewa penati za kutengeneza we ulitegemea nini?
Hata spain kwa mtindo ule lazima wafungwe tuu, jamaa ile mechi ya kwanza iliwasitua sana wakafanya maandalizi ya polini na ndio matokeo yake, usipende kujidharau unajua na wala hatukufungwa kwamba hatujui na ndio rushwa inayopigwa michezoni na ndio hayo mabadiliko wakubwa wanataka kufanya fifa, yaani acha anayejua na ashinde kihalali.
Mechi ya leo naweza kuchukulia unaenda kupigana na mwenzio alafu wewe mikono imefungwa kwa nyuma unategemea nini? Ile caf inahitaji mabadiliko labda unitafute nikuelezee, wewe tanzania uko kwenye kushindana mwenzako anataka matokeo na ujue kwa africa uwa hakunaga mwakilishi wa kweli kwenye world cup kwani kilichotokea kwao algeria cameroun ivory coast na ghana ni aibu na mwisho wa siku ni hao hao watakuwa wawakilishi wetu.
Na wazungu ukiwatajia mpira africa wanawataja hao kumbe kuna timu zina uwezo ila hazipati nafasi kwani caf yote ina milikiwa na francofone au french speaking country we kama ujui njoo nikueleze sio unazungumza utumba kwakuwa unasehemu ya kusemea inatakiwa tukae tusaidiane aibu ni yetu wote.
We unaleta masihara.