Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Una mawazo hasi sana kijana wangu
 
Swali la kitoto sana hili
Wewe chiku mbona unakua mnaa? Wewe unadhani miaka yooote hii tangia tumepata uhuru hatukuliona hilo swala la vazi la taifa??

Kuungunisha makabila 130+ kuwa taifa moja sio jambo dogo, kunahitaji upeo wa kipekee na kutoa sadaka baadhi ya vitu vya kipuuzi vinavyochochea ukabila kama vile mavazi ya kikabila kuwa 'vazi la taifa'.

Hakuna vazi la taifa, hautaki unaacha.
 
Pwani jee?mbeya jee?mara na bukoba na mwanza jee vipi kwa upande wa nchi ya Zanzibar?
 
Mnaa maana yake nini?
 
DRC wamerahisisha san. Wao wanakitambaa ( Kitenge) chenye utambulisho wa DRC, kuna rangi za bendera blue ikiwa imekolea zsidi na viashiria vingine kihusu taifa hilo.

Hicho kitambaa sababu kimetengenezwa maalum hukiti kama hicho na viashiria vyake huko china au nchi nyingine.

Walichoruhusu wao ni kila mtu kushona dizain anayoona inampendeza iwe shati , suruali, kilemba,koti, n.k.

Ni rahisi wao kutambuana hata akivaa juu shati la kitambaa kile na chini jeans .
 
Kuungunisha makabila 130+ kuwa taifa moja sio jambo dogo, kunahitaji upeo wa kipekee na kutoa sadaka baadhi ya vitu vya kipuuzi vinavyochochea ukabila kama vile mavazi ya kikabila kuwa 'vazi la taifa'.
Mbona Dodoma ndio mmepafanya kuwa makao makuu ya taifa? Kwani hilo haliwezi kuchochea ukabila? Makao makuu ya Serikali ilikuwa Dar (Kwa Wazaramo) sasa mmeamua kuihamishia Dodoma (Kwa Wagogo), unafikiri wazaramo wanajisikiaje kama issue ni ukabila?
 
Vazi la kimasai tayari ni vasi lililopasishwa na jamii kuwa vazi la kitaifa sijui serikali inasubiri nini kulipitisha kuwa la kitaifa, likifuatiwa na kanga na kitenge, japo ni mavazi ya Afrika nzima.
Msuko wa nywele ya masai nao unapendwa Tanzania nzima na dunia.
Waafrika huwa hatuchukui maamuzi ya haraka sijui kwa nini?
 
Mbona na wewe ideas zako ni kama za hao wahenga tu
Usipende kuwaza katika hali hasi bali chanya.Mbona kiswahili wabantu wa qaote wamekipokea kuwa lugha yetu rasm! Kumbuka wabantu babu yetu ni mmoja makabila ni koo mbalimbali za mbantu.
Umezikubali suti,kanzu ila hutaki vazi la ndugu yako bali la mwarabu na mzungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…