Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Moja huna unataka mbili we si mwehu
 
Nadhani hakuna kabila linalowakilisha jingine, mfano itamkwe kuwa vazi la Wagogo linawakilisha pia Wanyaturu, Wanyiramba au Warangi wakati si vazi lao. Pia mavazi ya Wamasai kuwakilisha Wachagga na Wapare wakati si mavazi yao.
Pia umetumia kigezo kipi kugawa kanda? hakuna Kanda ya Ziwa wala Kanda ya Nyanda za juu Kusini.

Anyway sidhani kuwa hii inaweza kuwa priority, labda kwa wabunifu wa mavazi iwe fursa.

Wengi wanavaa na tunavaa mitumba hasa jeans. Jeans ni kama vazi la taifa bila kulazimishana. Linatosha tu.
 
Nadhani hakuna kabila linalowakilisha jingine, mfano itamkwe kuwa vazi la Wagogo linawakilisha pia Wanyaturu, Wanyiramba au Warangi wakati si vazi lao. Pia mavazi ya Wamasai kuwakilisha Wachagga na Wapare wakati si mavazi yao.
Mbona Dodoma ndio makao makuu ya nchi wakati ndio chimbuko la kabila la wagogo na mengine kadhaa wakati mikoa mingine haijateuliwa na kupewa hadhi hiyo?
 
Kwani hao Wanyaturu, Wanyiramba, Warangi, Wamasai, Wachagga na Wapare, Dodoma ni mkoa wa asili yao? Mbona sasa ndio makao makuu ya taifa lao?...
 
Pia umetumia kigezo kipi kugawa kanda? hakuna Kanda ya Ziwa wala Kanda ya Nyanda za juu Kusini.
Kuna pande kuu nne za dunia mkuu. Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini. Hizo nyanda za juu kusini ni sehemu za kusini na hao kanda ya ziwa wangeitwaje kama kusingekuwa na hilo ziwa? Hao ni kaskazini tu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…