Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KabisaaaKuna mambo Dunia ya leo hayana maana tena, hili nalo ni moja wapo.
Kuyavaa makazini au nyumbani yote sawa tuWazo zuri. Ila kuvaa iwe option wasije lazimisha kila Ijumaa tuyavae makazini.
Naaam hakika umesema la maanaUzi ungenoga kama ungeweka na picha ya kila vazi ulilolipendekeza.
Ninywe kwa niaba yake?Soldier, kunywa beer nakuja kulipa. Wazo bora sana hili.
Mzee baba vaa kiasili utokelezeeKabisaaa
Ova
Kulazimishana jau mkuuMkuu, wahenga waliwahi kusema ya kuwa "hiyari yasinda utumwa". Hivyo, mtu akivaa kwa kupenda kila ijumaa itafaa zaidi kuliko kulazimishana.
Weka tena sasa hivi mzee babaSawa ngoja niweke picha nyingi zaidi
You can't be seriousKuna mambo Dunia ya leo hayana maana tena, hili nalo ni moja wapo.
Moja huna unataka mbili we si mwehuMambo vp jamiiforums.
Ninashauri sana nchi yetu ya Tanzania isiwe na vazi moja tu la taifa. Tuwe na mavazi rasmi matano (5) kutoka katika makabila yetu yatakayorasimishwa na kupewa hadhi ya utaifa. Yaaani kama inawezekana mpangilio uwe hivi au hata kama kura ya maoni inaweza kupigwa itakuwa sawa tu.
Picha hapo chini ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne mzee Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwa wamependeza vizuri kabisa katika mavazi ya kabila ya Waha (baba) pamoja na Maasai (Mama)
=====
View attachment 1718602
(1) Kaskazini - Vazi la kimaasai (Mkoa Arusha)
(2) Kusini - Vazi la Kimakonde (Mkoa Mtwara)
(3) Mashariki - Vazi la Kisambaa (Mkoa Tanga)
(4) Magharibi - Vazi la Waha (Mkoa Kigoma)
(5) Kanda ya kati - Vazi la wagogo (Mkoa Dodoma)
Nchini Afrika ya kusini wamefanya hili kwa upande wa lugha rasmi za taifa, ila sisi tunaweza kufanya hivi hivi kwa upande wa vazi rasmi la taifa.
Kwa uhalisia tu ni kwamba, huko nchini Afrika ya Kusini kuna makabila mengi sana yaliyopo katika majimbo tofauti tofauti na matokeo yake lugha zinatawala katika majimbo yao husika ambayo inafanya kuwa lugha mahususi haswa kwa eneo/mkoa husika.
Takribani lugha thelathini na tano (35) zenye asili ya Afrika Kusini huzungumzwa katika nchi hiyo, kumi kati ya hizo ni lugha rasmi za taifa la Afrika Kusini: Ndebele, Pedi, Sotho, Swati, Tsonga, Tswana, Venda, Xhosa, Zulu na Afrikaans.
Lugha rasmi ya kumi na moja ni Kiingereza, ambayo ndiyo lugha ya msingi inayotumiwa katika mazungumzo ya kibunge na kiserikali, ingawa lugha zote rasmi zina uzito sawa katika hadhi ya kisheria na katika ya nchi hiyo.
Kama katika lugha 35 kutoka nchi nzima waliweza kuchagua lugha 11 tu kutambulika kama "official languages" na Tanzania yenye makabila takribani 120 pia inaweza kuchagua mavazi kutoka makabila 5 tu kuwa ndio mavazi rasmi ya taifa ili tumalizane na hili suala kwa maana tangia lianze kujadiliwa ni zaidi ya miaka 15 sasa na bado sijaona solution ya maana mpaka sasa.
Soma pia>>> Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu duniani isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mzee wa funguo za BMWWazo zuri. Ila kuvaa iwe option wasije lazimisha kila Ijumaa tuyavae makazini.
NIACHE 😂😂😂Mzee wa funguo za BMW
Hayana umuhimu kabisa Tena ndio chanzo Cha ubaguz wa kikabilaKuna mambo Dunia ya leo hayana maana tena, hili nalo ni moja wapo.
Mbona Dodoma ndio makao makuu ya nchi wakati ndio chimbuko la kabila la wagogo na mengine kadhaa wakati mikoa mingine haijateuliwa na kupewa hadhi hiyo?Nadhani hakuna kabila linalowakilisha jingine, mfano itamkwe kuwa vazi la Wagogo linawakilisha pia Wanyaturu, Wanyiramba au Warangi wakati si vazi lao. Pia mavazi ya Wamasai kuwakilisha Wachagga na Wapare wakati si mavazi yao.
Kwani hao Wanyaturu, Wanyiramba, Warangi, Wamasai, Wachagga na Wapare, Dodoma ni mkoa wa asili yao? Mbona sasa ndio makao makuu ya taifa lao?...Nadhani hakuna kabila linalowakilisha jingine, mfano itamkwe kuwa vazi la Wagogo linawakilisha pia Wanyaturu, Wanyiramba au Warangi wakati si vazi lao. Pia mavazi ya Wamasai kuwakilisha Wachagga na Wapare wakati si mavazi yao.
Pia umetumia kigezo kipi kugawa kanda? hakuna Kanda ya Ziwa wala Kanda ya Nyanda za juu Kusini.
Kuna pande kuu nne za dunia mkuu. Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini. Hizo nyanda za juu kusini ni sehemu za kusini na hao kanda ya ziwa wangeitwaje kama kusingekuwa na hilo ziwa? Hao ni kaskazini tu mkuu.Pia umetumia kigezo kipi kugawa kanda? hakuna Kanda ya Ziwa wala Kanda ya Nyanda za juu Kusini.
Asante kwa mtazamo wakoWengi wanavaa na tunavaa mitumba hasa jeans. Jeans ni kama vazi la taifa bila kulazimishana. Linatosha tu.
Tanga ipo Mashariki mkuuHivi Tanga ipo Mashariki au Kaskazini? Na vazi la kisambaa huwa ni Vikoi au?