Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Tanzania haihitaji mavazi ya Taifa
Tanzania inahitaji mkakati wa kuwafanya wananchi wake specifically vijana kuwa na skills za kimaendeleo katika nyanja za sayansi na ufundi.
Nchi iwe ya wazalishaji hasa sio wachuuzi wa mitaani wanajaza barabarani bidhaa zenye viwango hafifu vya asia mashariki
Watu wawezeshwe kutengeza bidhaa ndogo ndogo za small scale industry kama Jua Kali Kenya
Sio kujaa mitaani kuuza vazi la taifa kwa vitambaa vinatoka China.
 
Tanzania haihitaji mavazi ya Taifa
Tanzania inahitaji mkakati wa kuwafanya wananchi wake specifically vijana kuwa na skills za kimaendeleo katika nyanja za sayansi na ufundi.
VETA pamoja na vyuo vingine kadhaa vya ufundi vipo na ndio vinavyofanya haya uliyoyaandika hapa. Unataka nini tena mkuu?...
 
Tanzania haihitaji mavazi ya Taifa
Tanzania inahitaji mkakati wa kuwafanya wananchi wake specifically vijana kuwa na skills za kimaendeleo katika nyanja za sayansi na ufundi.
Nchi iwe ya wazalishaji hasa sio wachuuzi wa mitaani wanajaza barabarani bidhaa zenye viwango hafifu vya asia mashariki
Watu wawezeshwe kutengeza bidhaa ndogo ndogo za small scale industry kama Jua Kali Kenya
Sio kujaa mitaani kuuza vazi la taifa kwa vitambaa vinatoka China.
Kwanini vitambaa visitoke China katika dunia ya sasa ya free market/globalization?

Alafu kumbuka kuwa China ni washirika wetu wa kimaendeleo.
 
Mambo vp jamiiforums.

Ninashauri sana nchi yetu ya Tanzania isiwe na vazi moja tu la taifa. Tuwe na mavazi rasmi matano (5) kutoka katika makabila yetu yatakayorasimishwa na kupewa hadhi ya utaifa. Yaaani kama inawezekana mpangilio uwe hivi au hata kama kura ya maoni inaweza kupigwa itakuwa sawa tu.

Picha hapo chini ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne mzee Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwa wamependeza vizuri kabisa katika mavazi ya kabila ya Waha (baba) pamoja na Maasai (Mama)
=====
View attachment 1718602

(1) Kaskazini - Vazi la kimaasai (Mkoa Arusha)

(2) Kusini - Vazi la Kimakonde (Mkoa Mtwara)

(3) Mashariki - Vazi la Kisambaa (Mkoa Tanga)

(4) Magharibi - Vazi la Waha (Mkoa Kigoma)

(5) Kanda ya kati - Vazi la wagogo (Mkoa Dodoma)

Nchini Afrika ya kusini wamefanya hili kwa upande wa lugha rasmi za taifa, ila sisi tunaweza kufanya hivi hivi kwa upande wa vazi rasmi la taifa.

Kwa uhalisia tu ni kwamba, huko nchini Afrika ya Kusini kuna makabila mengi sana yaliyopo katika majimbo tofauti tofauti na matokeo yake lugha zinatawala katika majimbo yao husika ambayo inafanya kuwa lugha mahususi haswa kwa eneo/mkoa husika.

Takribani lugha thelathini na tano (35) zenye asili ya Afrika Kusini huzungumzwa katika nchi hiyo, kumi kati ya hizo ni lugha rasmi za taifa la Afrika Kusini: Ndebele, Pedi, Sotho, Swati, Tsonga, Tswana, Venda, Xhosa, Zulu na Afrikaans.

Lugha rasmi ya kumi na moja ni Kiingereza, ambayo ndiyo lugha ya msingi inayotumiwa katika mazungumzo ya kibunge na kiserikali, ingawa lugha zote rasmi zina uzito sawa katika hadhi ya kisheria na katika ya nchi hiyo.

Kama katika lugha 35 kutoka nchi nzima waliweza kuchagua lugha 11 tu kutambulika kama "official languages" na Tanzania yenye makabila takribani 120 pia inaweza kuchagua mavazi kutoka makabila 5 tu kuwa ndio mavazi rasmi ya taifa ili tumalizane na hili suala kwa maana tangia lianze kujadiliwa ni zaidi ya miaka 15 sasa na bado sijaona solution ya maana mpaka sasa.

Soma pia>>> Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu duniani isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Wewe umesha chanjwa Corona???

Badala ya kushauri serikali na wataalamu kutafiti chanjo ya Covid wewe upo na nguo tu, kwani wewe leo huna nguo za kuvaa kama walivyokuwa babu zako mwaka 1900 ???.
 
Kwanini vitambaa visitoke China katika dunia ya sasa ya free market/globalization?

Alafu kumbuka kuwa China ni washirika wetu wa kimaendeleo.
Kwanini tusitengeneze vitambaa vya hilo vazi wenyewe, China ni Neo New Economical Colonial Master
Mimi nakumbuka mama alikuwa anapika vitenge mwenyewe
Wakati huo kila mwananchi alikuwa na ile ari ya kujitegemea
Na SIDO ilijaribu lakini wezi wakaja kula kila kitu
Hata Shillingi ilikuwa inajibeba kwenye currency market

Mkuu achana hizi stori za mafuta ya mpako
Hamasisha micro development tusiwe nchi ya wachuuzi
 
Kwanini tusitengeneze vitambaa vya hilo vazi wenyewe
Mbona viwanda vipo kama KTM Mbagala na kile cha Morogoro. Mbona kuna akina mama wapo chini ya uangalizi wa SIDO pia wanafanya vizuri tu katika viwanda vyao vidogodogo...
 
South Afrika kuna makabila mangapi? Je kuna kabila lolote ambao wameachwa kwa lugha yao kutokutambulika??
Makabila yapo 37 ila lugha rasmi ni 11, sasa wewe hauoni hapo kama kuna makabila mengine yameachwa na hawakuleta migogoro yoyote?
 
Back
Top Bottom