Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Katika ziara ya Rais wa Zambia nchini Tanzania, Mh Hakainde Hichilema July 2, 2022, yeye na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania walikubaliana kufufua ujenzi wa reli ya kihistoria ya TAZARA kwa kiwango cha ‘Standard Gauge Railway’ (SGR). Reli ya TAZARA ina urefu wa kilomita 1,860.
Binafsi nina mtazamo na maono chanya sana kuhusu uamuzi wa serikali hizi mbili kujenga reli hii. Mimi kama Mtanzania, naiona reli hii kama fursa kubwa katika kuchochea maendeleo katika sekta zifutatazo nchini, nazo ni, usafirishaji, kilimo, utalii pamoja na sekta ya bandari.
KILIMO
Kupita bajeti ya Wizara ya Kilimo 2022/23 Serikali imeazimia kujenga viwanda vikubwa vitatu vya kuchakatia nafaka mbalimbali nchini. Viwanda hivyo vitajengwa Mbeya, Dar es Salaam na Mwanza. Mbeya ni eneo ambao reli ya TAZARA imepita, hii ni fursa kwa Tanzania kwani itaweza kusafirisha bidhaa kwa shehena kubwa zaidi kupitia reli kwenda katika mikoa mingine na nchi jirani, hivyo kuliongezea taifa mapato. Usafirishaji kwa reli hubeba shehena kubwa zaidi kuliko usafirishaji wa mabasi.
Viwanda cha Chunya-Mbeya ambacho kazi yake ni kukoboa mpunga, kitanufaika sana kutokana na urahisi wa usafiri wa bidhaa hiyo kwenda nje ya nchi, na pia mikoa ya jirani.
Kupita reli hii, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kupunguza bei za usafirishaji hivyo kuimarisha kilimo pembezoni na katika mikoa/sehemu zinayopitiwa na reli kama Iringa, Mbeya, Tunduma, Makambako ambako kote huku, bidhaa zinaweza kusafishwa kwa muda mfupi na kwa wingi zaidi hivyo kuliongezea taifa mapato maradufu zaidi.
Reli hii inaweza kutumika kusafirisha shehena za mbolea kwa wakulima ndani ya muda mfupi, kwa urahisi na kwa gharama nafuu zaidi.
UTALII
Sekta ya Utalii inakuwa kwa kasi sana chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Hii hasa ukizingatia na kufunguliwa kwa mipaka ya nchi nyingi baada ya kupungua kwa janga la UVIKO-19 duniani.
Reli hii itatumika kusafirisha watalii kwenda Udzungwa, Selous na Mikumi kwa Urahisi zaidi na kupunguza gharama za usafiri hasa kwa watalii. Usafiri wa treni hutoa burudani ya tofauti na fursa ya kipekee ya kuona vivutio vingi kwa kutokana na uhalisia kwamba reli imekatiza katika maeneo mbalimbali yenye mabonde yenye maporomoko yakuvutia, milima, mabonde pamoja na mapori mazuri.
USAFIRISHAJI
Abiria waendao mikoa ya Mbeya, Morogoro, Iringa na kadhalika watapata mbadala wa usafiri kutokana na usafiri unaotumika sasa kwa sasa ni mabasi tu. Kutumia treni kama njia kuu ya usafirishaji kutapunguza muda idadi ya magari barabarani hivyo kupunguza uharibifu wa barabara na kuzifanya zidumu muda mrefu zaidi.
BANDARI
TAZARA haitohudumia Tanzania na Zambia pekee, kuna mataifa kama Malawi, Zimbabwe na kadhalika ambayo yanaweza kupitisha mizigo yao kupitia bandari ya Dar es Salaam na shehena za mizigo hiyo kusafirishwa kwa reli ya TAZARA kuelekea nchi hizo. Haina maana reli inafika hadi kwenye hizo, ila ni rahisi shehena hizo kusafirishwa kwa reli hadi Zambia, kisha kufaulishwa na kupelekwa kwenye mataifa hayo. Hii italiingizia taifa mapato yakutosha na kuimarisha sekta ya Bandari nchini.
Itoshe tu kusema kwamba hakuna wakati ambao tunamuhitaji sana Rais Samia Suluhu kama wakati huu. Hakika haya ni maono ambayo pengine, tuliyahitaji miaka 10 nyuma, lakini Mungu alitupima subira zetu kwa wakati wote huo, akijua kwamba wakati sahihi utafika, na wakati wenye ndio huu, chini ya Mama, Rais Samia Suluhu Hassan.