Tanzania itapata faida gani kama TAZARA itajengwa kwa kiwango cha SGR?

Reli iliyopo imeshindwa kutimiza hayo yote?
 
Kwenye utekelezaji na customer service sisi ni wababaishaji wa kutupwa. Porojo nyingi vitendo hakuna. Hakuna hata kitu kimoja tunachofanya kwa ufanisi
Siasa mingi, ndio kama hiya tunayoambiwa double lane , wakati reli mnaacha inaozeana , hatuna planning kabisa, tunaenda na utashi wa aliyekuwepo
 
..kwa taarifa yenu asilimia 83 ya reli za JAPAN ni za gauge sawa na ya Tazara, Cape Gauge.

..mwaka 2019 Angola walikamilisha ukarabati ya reli ya Benguela yenye urefu wa kilomita 1300++.

..sioni ulazima wa kubadilisha reli ya Tazara toka Cape Gauge kwenda Standard Gauge.
 
Naungana nawe mkuu, nchi yetu tunahitaji tuchukue mizigo ya DRC even for 45%,tutatengeneza fedha nyingi mno, DRC (the future economic giant ya Africa)mizigo yake mingi inakwenda Walvis bay, Durban ambako ni mbali sana, inatakiwa ije Dar
Sawa. Kuanzia Leo hiyo mizigo yote ya DRC ipite Dar (Signed).
 
Rilway police wana kazi gani? Reli ni muundombinu kama miundombinu mingine. Inalindwaje?
Kweni hata Tazara si ilikuwa na lengo hilo hilo yako wapi?

SGR ya Ethiopia imebaki story tu huku Malori yakipeta.
 
Mkuu wazambia walikuwa wanaitumia sana hio reli kupitisha mizuho kutoka bandarini tena hata Botswana, ila baada ya kutoka wizi sana pale bandarini kipindi cha mkweli, na mkweli kujiingiza kwenye biashara ya malori reli ndo ikafa.
 
Watu wengi wanadhani kuwa kujenga SGR ndiyo suluhisho la matatizo yote ya usafirishaji kwa reli.
Wanashindwa kuelewa kuwa kujenga SGR ni jambo moja, na uendeshaji kwa ufanisi ni jambo jingine.

Hizi reli tulizo nazo sasa tunaziendesha kwa ufanisi chini ya asilimia 25.

Kama tunashindwa kuendesha hizi reli tulizo nazo kwa ufanisi, tutawezaje kuendesha SGR kwa ufanisi? Muda ndiyo utatupa jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…