Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Tangu Rais wa Marekani, Donald Trump, alipotangaza viwango vipya vya ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo, kumekuwa na hofu kutoka kwa mataifa mbalimbali duniani ya jinsi yatakavyoathirika.
Wakati mataifa mengine kwa ujumla yakitangaziwa na Marekani ushuru wa jumla wa asilimia 10 tangu mwishoni mwa wiki, China imelimwa ushuru wa asilimia 104, hali inayoshiria ushindani mkali kati ya mataifa hayo mawili.
Kupandishwa kwa ushuru huo kulikotangazwa tangu Februari 2025, kumesababisha mauzo makubwa ya hisa katika masoko kote duniani na kuchochea hofu ya mdororo wa uchumi.
Ushuru huo mpya unalenga sekta mbalimbali, hasa kilimo na viwanda, ambazo zinategemewa na mataifa duniani kupata fedha za kigeni.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), anchokifanya Trump ni kuhakikisha nchi hiyo inanufaika zaidi, kwa sababu zipo nchi zinazoitoza bidhaa za Marekani kiwango kikubwa zaidi cha ushuru.
“Trump anasema hilo linakoma.”
BBC imechambua ushuru unaotozwa na nchi za Afrika Mashariki, ikionyesha nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa ndiyo inayotoza asilimia 22 kwa bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka Marekani, huku nchi nyingine zikitoza asilimia 10 tu.
Mataifa hayo ni pamoja na Tanzania inayotoza asilimia 10 kwa bidhaa zinazotoka Marekani na asilimia 10 kwa bidhaa zinazoingia Marekani kutoka Afrika Mashariki.
Nchi nyingine zinazotoza asilimia 10 kwa pande zote ni pamoa na Kenya,
Ethiopia, Rwanda, na Burundi, huku Uganda ikitoza asilimia 20 kwa bidhaa zianzotoka Marekani na asilimia 10 kwa bidhaa zinazotoka Marekani na DRC asilimia 22 kwa bidhaa zinazotoka Marekani na asilimia 11 kwa bidhaa inazopeleka Marekani.
Tutarajie maumivu
Akizungumza na Jamii Africa, mhadhiri wa uchumi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk Timothy Lyanga alisema ushuru huo una athari kubwa kwa nchi za Afrika hususani Tanzania.
“Unapoongeza kodi kwenye bidhaa tafsiri yake ni kwamba unaongeza bidhaa hizo na mamivu kwa mlaji. Vilevile ushuru huu unamaanisha kwamba nchi inayoeleka bidhaa nchini Marekani pia inaongezewa gharama, kwa hiyo hata sisi tumeongezewa gharama ya kupeleka bidhaa,” amesema.
Amesema hatua ya Trump kutangaza ushuru huo inakiuka makubaliano ya kibiashara kupitia Sheria ya Ukuzaji na Fursa kwa Afrika (AGOA), hata hivyo alisema makubaliano hayo hayajavunjika.
“Hiyo inaathiri kubwa kwenye makubaliano ya AGOA ambako tulikuwa tukishafirisha bidhaa bila kulipa ushuru, lakini yale makubaliano hayavunjiki hivi hivi kwa sababu ni ya kisheria, hivyo ni lazima mkae mezani mkubaliano vifungu vilivyovunjwa,” amesema.
Akifafanua athari zake, amesema ni pamoja na kupunguza uwezo Tanzania kupeleka bidhaa nchini Marekani na hivyo kupunguza uwezo wa kuingiza fedha za kigeni.
“Hali hiyo itapunguza uwezo wa kudhibiti mfumuko wa bei. Pia tutarajie kodi za ndani zitaongezeka,” amesema.
Ameongeza, “Kwa ujumla tutarajie maumivu na hivyo tuanze kufikiria masoko mengine kama China na Russia ambako hakuna viikwazo.”
China yatoa ahueni Afrika
Wakati maumivu hayo yakitarajiwa, China imetoa msamaha wa ushuru kwa asilimia 100 kwa nchi 33 za Afrika kwa bidhaa zao zote zinazoingia kwenye soko la nchi hiyo.
Uamuzi huo umetajwa kuimarisha nafasi ya China kama mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa mwaka wa 15 mfululizo, bali pia unaangazia umuhimu unaoongezeka wa uhusiano wa kibiashara kati ya China na Afrika.
Kwa miaka kadhaa sasa, sehemu ya biashara kati ya China na Afrika katika jumla ya biashara ya nje ya Afrika imeendelea kuongezeka, ikiashiria ushirikiano unaozidi kuwa wa kina kati ya pande hizo mbili.
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa China imeipita Marekani kama mshirika mkuu wa kibiashara wa Afrika. Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, mataifa ya Afrika yamezidi kuelekeza macho yao Beijing, yakivutiwa na ukubwa wa soko lake, fursa za uwekezaji, na miradi ya maendeleo ya miundombinu.
Mivutano ya kibiashara kati ya Marekani na China inatajwa kuwa na athari kwa mataifa ya Afrika na duniani kote.