Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Huko nyuma tuliwahi kusema kuwa "kila mtu anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Pia tulisema kwamba kila watu wana haki ya kuwa na mahali ambapo watakuwa salama kutoka vitisho vyovyote vya utu wao na nafasi yao kama jamaa.
Kwa sababu hiyo tuliunga mkono POLISARIO na PLO, kama vile tulivyounga mkono Biafra, kuunga mkono ANC, FRELIMO n.k Tuliamini ya kwamba hakuna mwanadamu mwingine ambaye ana haki ya kumtawala kwa nguvu mwanadamu mwingine kwa kisingizio chochote kile. Hii ilikuwa ni falsafa yetu dhidi ya ukoloni.
Leo hii tunashuhudia yanayoendelea Palestina ambapo karibu maelfu ya watu wameshauawa. Je, Bunge linapokutana siku chache zijazo zilaani mauaji hayo? Je serikali ilaani pande zote mbili kwa kusababisha mazingira ambayo yanamnyima mwanadamu nafasi ya kuwa huru kufanya lolote? Je tuungane na nchi kama Venezuela na Bolivia ambazo zimevunja uhusiano na Israel kutokana na suala la Gaza?
Je tukifanya hivyo hatutaulizwa uhusiano wetu na nchi kama Sudan, Somalia, Iran, n.k ambapo rekodi zao kuhusu haki za binadamu na raia si za kupewa sifa?
Au tuendelee kukaa pembeni tu na kuwaacha "wafu wawazike wafu wao"?