Nashangaa waislamu wanavyoandamana Dar kwa vifo vya wapalestina wakati waislamu weusi wa Darfur wanauwawa kwa wingi huko Sudani ya kusini.Nawataka waache double stardard
Waarabu ni watu wa ajabu hawako pamoja na bara la Africa kwenye shida zao.Wakati Afrika ilikuwa ikiwashambulia makaburu wa Afrika ya kusini waarabu walikuwa wakiendelea kuwauzia mafuta bila kuungana na Africa lakini wakati huo huo walikuwa wakitaka Afrika iwaunge mkono waarabu wa Palestina dhidi ya Israeli.
Waislamu wa Somalia ambayo iko Afrika wanauawa kila siku lakini husikii cha maandamano wala nini nchi za kiarbu kupinga uharamia unaofanyiwa raia wa Somalia wasiokuwa na hatia wala huoni Televisioni ya Waarabu ya Aljazeera (ARJAZEERA TV) ukipenda waweza iita HAMAS TV ikitangaza habari za raia wanaouliwa Somalia na kuitisha jumuiya ya kimataifa au ya kiislamu iwasaidie wasomali wa Afrika wasio na hatia wanaouawa kila siku.Habari za mauaji zinazotangazwa na HAMAS TV (ALJAZEERA TV) ni zile za wapalestina wakati kuna waislamu wasomali wenye hali mbaya kuliko wapalestina kutokana na vita.
Pia Upande wa Sudan serikali ya mwarabu Omar al Bashir na maraisi waarabu waliomtangulia walikuwa wakiwaua wakristo weusi wasiokuwa waarabu wa Sudani ya kusini hakukuwa na maandamano yoyote ya nchi za kiarabu kulaani,kuandamana n.k kuwatetea wakristo hao weusi wa Sudan waliokuwa wakivurumishiwa makombora na serikali ya mwarabu wa Kartoum sudan.
Watu tukadhani kuwa Serikali ya mwarabu wa Sudan ilikuwa ikiwaonea waafrika weusi wa Sudan ya kusini sababu ni wakristo jumuiya ya kimataifa ikapiga kelele hadi tatizo likafikia mahali pa kupungua wakapata serikali yao.Ilipoona imeshindwa kuendelea kunyanyasa waafrika weusi wa Sudan Kusini Serikali ya Mwarabu wa Sudani ikawageukia waislamu weusi wa Darfur na kuanza kuwanyanyasa na kuwaponda kwa makombora na maroketi.Wakati hilo likiendelea hatukuona nchi yoyote ya Kiarabu wakiandamana kupinga uvamizi na mashambulizi ya makombora Mwarabu Omar al Bashir Raisi wa Sudan kwa wananchi waislamu weusi wa Darfur.Tunashukuru mahakama ya kimataifa kutoa hati ya kukamatwa kwa mwarabu Omar AL basher angalau nchi za magharibi zisizo za kiislamu zimeamua kutetea waafrika weusi waislamu wa Darfur wakati waislamu wa Uarabuni wamekaa kimya wakila tambuu na kashata kama vile wanaokufa Darfur ni ngedere wa porini.
Ninachokiona ni kuwa waarabu hawako pamoja na waafrika weusi katika taabu zao lakini wao wanataka waafrika weusi wawe nao katika taabu zao.Wepesi kuhamasisha misikitini watu walaani mashambulizi ya waarabu Palestina lakini si wepesi kuhamasisha watu misikitini waandamane walaani ya Somalia au Darfur.Hata TV yao ya HAMAS TV (aljazeera TV) inakesha usiku na mchana kwa siku nyingi mfulilizo inatangaza mauaji Palestina lakini haijawahi tumia hata siku moja mfululizo kutangaza vita na mauaji yanayoendelea Somalia,Sudan ,Kusini ,Wala Darfur.
Binafsi sioni sababu ya kuvunja uhusiano wa Kibalozi na Israeli sababu waarabu nao hawakuvunja uhusiano na serikali oneaji ya Sudan inayoonea waafrika weusi ila napendekeza uhusiano wa kibalozi na waarabu wa Palestina ndio tuvunje maana wapalestina hatujawahi ona wakiandamana kupinga mauaji ya Somalia,Sudan kusini wala Darfur wala kuvunja uhusiano na adui huyo wa waafrika weusi.
Sioni sababu ya kuendelea na uhusiano na watu ambao hawako na wewe kwenye misiba yako lakini wanataka wewe ulie machozi hadi ujinyee kwenye misiba yao.Shenzi type. Wapalestina hawatusaidii kwenye migogoro ya Sudan Kusini wala ya waislamu wa Darfur na Somalia.Hao watoto na wanawake wanaoonyeshwa Palestina wanaathirika kwenye TV na hiyo vita na Israeli wana nafuu ukilinganisha na wanawake na watoto wa Somalia,Sudan kusini,na Darfur ambao hawana TV kama ya HAMAS TV (Aljazeera TV) ya ku-market taabu zao kwenye soko la wasaidaji wa kimataifa au waona huruma wa kimataifa.
Msimamo wa Tanzania ungekuwa kukaa kimya kama Wapalestina wanavyokaa kimya kwenye migogoro ya Somalia,Sudan Kusini na Darfur.Wa Tanzania tuanze kuwa na misimamo kwenye medani za kimataifa siasa za kujikomba komba hazina nafasi kwenye utandawazi.Utanawazi unahitaji watu wababe wanaojua haki zao na nchi zao na wawezao kuzisimamia bila woga wala kumeza maneno iwe kwenye vikao vya kimataifa,siasa,biashara au uchumi wa nchi.