Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hii Nchi ni dhahiri sasa kwamba Wananchi wake wamechoka kuwaza , nadhani hali hii inatokana na dhiki zinazowakabili raia ikiwa ni pamoja na umasikini wa kutupwa pamoja na mgawo kabambe wa umeme .
Yaani kila mtu ambaye siyo Mtoto wa kiongozi akiteuliwa kushika wadhifa wowote anaonekana ni kutoka usalama wa Taifa! kwamba Raia yeyote ambaye ni mfanyakazi tu labda wa kiwanda cha Urafiki , KTM , UFI , au Mwalimu wa shule ya Msingi Mtakuja, Ikolo au Ibonde hana haki ya kuteuliwa , na ikitokea kateuliwa basi haraka tu anaitwa Kitengo.
Cha kuchekesha sasa Wateuaji wenyewe , mfano Rais na Mawaziri hawajawahi kuitwa Kitengo , au Watoto wa viongozi wakiteuliwa wao hawaitwi vitengo ila utasikia kwamba ni Koneksheni .
Hii Nchi aliyeiloga bila shaka alikuwa katili sana ! maana kailoga kuanzia Unyayo hadi nywele.
Poor Tanzania!