SoC03 Tanzania, Kitovu cha Hifadhi ya Historia ya Afrika na Utalii

SoC03 Tanzania, Kitovu cha Hifadhi ya Historia ya Afrika na Utalii

Stories of Change - 2023 Competition

LYN Writes

New Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Huezi kuizungumzia Afrika, pasipo kutaja Mlima mrefu zaidi, Mlima Kilimanjaro upatikanao nchini Tanzania. Huezi zungumzia Afrika, pasipo kuitaja Serengeti, hifadhi iliyopo nchini Tanzania na iliyoshinda tuzo ya hifadhi bora zaidi barani Afrika mara nne kwa mfululizo na huezi zungumzia Afrika pasipo kuitaja lugha adhimu inayozungumzwa Afrika mashariki, barani Afrika na ulimwenguni, lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo Lugha rasmi nchini Tanzania.

Hii ni kielelezo tosha ya namna nchi yetu ya Tanzania imezungukwa na utajiri asilia. Tukizungumzia Historia ya Tanzania na Historia ya Afrika wengi wataizungumzia kwenye jicho la utumwa lakini je hii ndio historia pekee tuliyonayo? Tuna historia Tajiri, historia ya watu waliyofanya vitu mahiri kabla ya ukoloni na baada ya ukoloni katika Nyanja mbalimbali kama vile uongozi na Sanaa. Je ni kwa namna gani tunaweza kuhifadhi na kuwekeza katika utajiri huu kwa vizazi vijavyo katika ulimwengu wa sasa?

Ulimwengu was sasa unatuhitaji sisi kuenenda na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia na hatuezi kufanya hivyo pasipo kuwa wabunifu na wenye weledi wa Elimu ya kidijitali. Kwakua Sanaa na ubunifu huwa vinashabihiana basi itoshe tu kusema tutaweza kuhifadhi historia yetu ikiwa Tutaunda Jukwaa la kidijitali litakaloenda kuzalisha maudhui kwa mfumo au filamu au tamthiliya zenye simulizi za urithi wetu kwa lengo la kukuza tamaduni zetu, kuburudisha na kuelimisha umma juu ya historia ya Tanzania na Afrika kiujumla”
photo_2023-07-26_17-44-24.jpg

African Art Gallery inapatakina Arusha, nchini Tanzania, gallery hii ni mjumuisho wa michoro, vinyago na tamaduni mbalimbali zinazoelezea historia ya Afrika.


Tuangazie makundi matatu ya watu watakaohitajika na faida za kuanzishwa kwa jukwaa hili nchini Tanzania

Kuanzisha jukwaa hili la kidijitali kutahitaji msingi wa makundi haya ya watu,
  • Wanahistoria​
Kwakua kazi yao kuu ni kuchambua, kurekodi, na kuelimisha kuhusu matukio ya kale na mabadiliko ya jamii. Hivyo basi wanapaswa kuwa na ufahamu wa kina wa muktadha wa kihistoria, wanapaswa kufanya uchambuzi wa kina juu ya athari za matukio ya zamani kwa sasa. Kupitia machapisho yao na maandishi, wanaweka mchango muhimu katika kukuza utamaduni wa kuheshimu na kuenzi historia na kuifanya ipatikane kwa vizazi vijavyo.​
  • Waandishi​
Waandishi au kwa lugha ya kiingereza “Script Writers”hujenga hadithi za kusisimua na mazungumzo ya kuvutia katika kazi zao za sanaa na hujitahidi kuelewa hadhira na lengo la kazi ya sanaa wanayoandika ili kutoa ujumbe unaofaa na unaogusa hisia za watazamaji.​
  • Watayarishaji wa filamu​
Hawa ndio wanaosimamia kila hatua ya uzalishaji, hushirikiana na wahariri wa filamu kuhakikisha kuwa sehemu zote zinaunganishwa vizuri na kupata muundo mzuri wa hadithi.

Faida za kuwepo kwa jukwaa hili la kidijitali
  • Tanzania itakua kitovu cha hifadhi ya Historia ya Afrika, uwepo wa jukwaa hili utasaidia kurusha maudhui zenye kusimulia tamaduni zetu nchini na Afrika kiujumla. Filamu na Tamthiliya hizi zitaigizwa kwa kuzingatia tamaduni na watu wa nchi husika, filamu hizi zinaweza kuhusu matukio mbalimbali au watu mahiri waliyowahi kutokea. Zinaweza zikagusia moja ya kiongozi tajiri zaidi ulimwenguni kutoka Afrika Magharibi Mfalme Mansa Musa wa Mandinga, au Mwanamziki maarufu Afrika Mashariki Siti Binti Saad, au Malkia Nzinga wa Ndongo na Matamba aliyesimamisha utumwa wa watu wake dhidi ya Wareno. Ukweli ni kwamba Historia ipo na ni nyingi tunahitaji jitihada za kutosha katika kuhifadhi utajiri huu.​
  • Kukuza utalii nchini, Tanzania itakua kitovu cha matangazo ya kitalii barani Afrika, jukwaa hili halitoishia kwenye uzalishaji na usambazaji wa filamu na tamthiliya hizi za kihistoria bali pia itakua ni sehemu ya kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo barani Afrika.​
  • Itakuza uchumi wa nchi, kwa kila filamu au tamthiliya itakorushwa ndani ya jukwaa, mtazamaji itabidi alipie kiasi cha fedha kwa kipindi cha muda flan, na malipo haya yatafanyika kupitia mifumo mbalimbali ya malipo iliyopo.​
  • Itakuza Lugha ya Kiswahili, jukwa hili litanedeshwa kwa lugha mbili yaani Kiswahili na Kiingereza, licha ya hizi kua ndio lugha kuu hii haina maana ya kwamba filamu kutoka nchi nyingine hazitorushwa kwa lugha zao asilia, filamu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika zitakua na lugha zao lakini kutakua na uhuru wa kuchagua majalada ya maandishi yaani subtitles za Kiswahili au Kiingereza​
  • Itakuza Elimu katika ngazi tofauti, Watoto wa shule za msingi watapata fursa ya kujifunza na kujua historia yao katika mfumo wa masimulizi yenye kuburudisha, vivyo hivyo kwa vijana na watu wazima. Kwa upande wa wazee wataweza kukumbushwa juu ya Historia ambayo ilikua imeshasahaulika machoni pao​
  • Itaimarisha umoja na ushirikiano baina ya mataifa ya Afrika, uzuri ni kwamba jukwaa hili halitoweka kikomo cha hadhira yake kwakua kila stori ya Afrika inapaswa kusimuliwa na Waafrika na kama kuna jukwaa hususan kwa ajili ya hilo kwanini watu katika tasnia ya Sanaa kutoka mataifa barani Afrika wasilete kazi zao ili zirushwe katika jukwaa hili.​
Ni hakika kuwa jukwaa hili litaenda kuleta mabadiliko katika tasnia ya Sanaa na jitihada hizi haziwezi kukamilika pasipo ushirikiano wa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Tunaamini kwa kuzalisha filamu na tamthiliya zenye maudhui ya aina hii kutasaidia katika kuzungumzia na kuibua masuala mbalimbali ambayo kama jamii ya sasa inakumbana nayo, kama vile Elimu juu ya afya ya akili, kupinga unyanyasaji dhidi ya mwanamke, umuhimu wa elimu jumuishi, umuhimu wa uwazi na uwajibikaji kwa jamii inayotuzunguka. Siwezi kumaliza andiko hili pasipo kuyaenzi maneno ya busara ya Baba wa Taifa hili la Tanzania.

“Kosa jingine ni kutojielimisha. Kanuni yetu moja inasema: Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.” BABA WA TAIFA MWALIMU J.K NYERERE
 
Upvote 0
Back
Top Bottom