Ngurdoto Hotel aisee, assets (buildings) wanazo sasa sijui Management na Business Manager wa Ngurdoto wamewaza nini mpaka kukubali kuifanya iwe Hostel za wanafunzi kwa gharama ya Tsh. 400,00/- kwa mwaka.
Sasa si bora wamiliki wa hii 5-star hotel wangeitangaza upya kibiashara kwa kuifanya iwe tu kama Lodge (guest house) ya bei chee ambayo wangekula Tsh. 12,000/- kwa siku kwa kila chumba kimoja.
Hivyo chumba kimoja tu kingekuwa na uwezo kuingiza karibia Milioni 4 kwa mwaka.
Tsh. 12,000 x siku 365 = Tsh. 4,380,000/- kwa mwaka kwa chumba kimoja.
Sasa sijui wanavyo vyumba vingapi jumla, Maana hapo makadirio niliyopiga ni ya chumba kimoja tu.
Na kwa hadhi ya brand ya Ngurdoto, kibiashara kwa model wangefaidika zaidi maana resources muhimu (buildings) wanazo tayari.
Anyway, sijui lengo la wamiliki haswa ni lipi.