DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter *******, amewapokea wageni kutoka Hospitali ya Apollo ya India waliotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya tiba utalii na huduma za kibingwa.
Dkt. ******* amesema kuwa JKCI imeanzisha rasmi huduma za Tiba Utalii, zitakazowahusisha watu mbalimbali kutoka nje ya Tanzania kuja kupata matibabu ya moyo na huduma nyingine za kibobezi nchini.
Katika ziara hiyo, mmoja wa madaktari bingwa kutoka Apollo Hospital amewezesha upasuaji wa moyo kwa njia ya tundu dogo (minimal invasive surgery) njia ambayo nchini Tanzania tulikuwa tinatekeleza kwa namna nyingine.
"Daktari huyu amefanikisha upasuaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa, badala ya upasuaji mkubwa tuliozoea kutumia hapa nchini. Hii ni hatua kubwa kwa JKCI na kwa sekta ya afya kwa ujumla," alisema Dkt. *******.
Aidha, ameeleza kuwa taasisi hiyo iko mbioni kuangalia uwezekano wa kufanya upasuaji kwa kutumia roboti, ikiwemo upandikizaji wa moyo na matibabu ya matatizo ya "heart attack".
"Tutaendeleza ushirikiano huu mzuri na wenzetu wa Apollo ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora zaidi za afya, bila kulazimika kusafiri nje ya nchi," aliongeza.