ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
Tanzania imefanya mazungumzo ya makubaliano makubwa ya kuiuzia Zambia umeme wa hadi megawati 1000 kwa mwaka, kupitia mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kanona Power (T) Limited, kampuni tanzu ya Kanona Power Company Limited kutoka Zambia.
Ikiwa mazungumzo hayo yatafanikiwa, basi mkataba utakaosainiwa unatarajiwa kuingizia TANESCO mapato ya takriban Dola bilioni 1 (TZS trilioni 2.5) na kuongeza mchango wa sekta ya nishati kwenye uchumi wa Tanzania.
Aidha, ikiwa mazungumzo hayo yatafikia makubaliano, Kanona Power itajenga njia ya kusafirisha umeme ya kV 220 kutoka Mwakibete, Mbeya hadi Nakonde, mpakani mwa Tanzania na Zambia. Hatua hii inalenga kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa wakati huku ikisaidia mahitaji makubwa ya nishati kwa nchi jirani.
Halikadhalika Kanona Power, ambayo kwa sasa inasambaza umeme kwa kampuni kubwa ya madini nchini Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), inatarajia kuanza kununua umeme kutoka TANESCO kwa awamu, ambapo megawati 100 za kwanza zitaanza kuingizwa katika mwaka wa fedha wa 2025/2026 mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya kV 220.
Usambazaji wa umeme zaidi utafanyika baada ya kukamilika kwa mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa kV 400 wa Tanzania-Zambia (TAZA), unaotarajiwa kukamilika mwaka 2026 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba aliyoitoa kwa wanahabari siku tisa zilizopita wakati akizungumza na wanahabari kutolea ufafanuzi hoja ya Tanzania kununua umeme kutoka Ethiopia.
Wakati akitoa ufafanuzi huo, Mhandisi Mramba aligusia pia Tanzania kupanga kuiuzia umeme Zambia, akitanabaisha kuwa kampuni ya migodi kutoka Zambia ambayo ni Kanona Power ipo katika mazungumzo ya kuhitaji megawati 1000 huku Serikali ya Zambia ikiwa na uhitaji wa kuuziwa megawati 600.
Hatua hii imetajwa kuwa muhimu kwa TANESCO, siyo tu kwa ajili ya kuongeza mapato, bali pia kuimarisha nafasi ya Tanzania kama mzalishaji mkubwa wa umeme katika ukanda wa Kusini na Afrika Mashariki.