Tanzania kuendelea na Mkataba wa Adani wa Dola Milioni 95 kuendesha Gati za Bandari ya Dar Licha ya Tuhuma za Rushwa

Tanzania kuendelea na Mkataba wa Adani wa Dola Milioni 95 kuendesha Gati za Bandari ya Dar Licha ya Tuhuma za Rushwa

Duh!

Kiukweli ipo siku hawa wanasiasa wetu atatokea kiongozi mwingine kama JPM atawanyonga wote-tuanze upya! Huwezi ukawa na akili au nia njema na watu wako ukafanya maamuzi kama haya! No way.
Hapo ni maamuzi gani mabaya yamefanywa au ndio hasira za kushindwa Uchaguzi
 

Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuheshimu mikataba yake na kampuni tanzu ya Adani Group licha ya mashtaka mapya dhidi ya Gautam Adani, mwenyekiti bilionea wa kundi hilo, anayekabiliwa na tuhuma za utoaji hongo na udanganyifu, afisa mwandamizi wa Mamlaka ya Bandari amethibitisha.

Wiki iliyopita, Adani na mpwa wake walikabiliwa na mashtaka ya udanganyifu na hati za kukamatwa zilitolewa dhidi yao, wakituhumiwa kupanga njama ya dola milioni 265 kuwahonga maafisa wa India ili kupata mikataba ya usambazaji wa umeme. Hata hivyo, Adani Group imekana tuhuma hizo.

Mwezi Mei, Tanzania ilisaini mkataba wa miaka 30 na Adani Ports, kampuni tanzu ya Adani Group, kuendesha Gati ya Makontena 2 katika Bandari ya Dar es Salaam. Mkataba huo pia ulijumuisha ununuzi wa asilimia 95 ya hisa za Kampuni ya Huduma za Gati za Makontena za Kimataifa ya Tanzania (TICTS) kwa dola milioni 95.

"Hatujakuwa na matatizo na mtu yeyote. Shughuli zetu zote zinafanywa kwa mujibu wa sheria na makubaliano yetu," alisema Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, alipoongea na Reuters Jumanne. Alisisitiza kuwa Tanzania haikabiliwi na madai yoyote ya udanganyifu kuhusu mikataba yake. "Kama kuna watu wengine wanachukua hatua, basi wanachukua kwa sababu zao."

Wakati huohuo, nchini Kenya jirani, Rais William Ruto hivi karibuni alifuta mkataba wa Adani wa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme. Pia alikataa mapendekezo ya kuongeza barabara ya pili ya ndege na kuboresha kituo cha abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, mpango ambao ungehusisha mkataba wa upangaji wa miaka 30.

PIA SOMA
- Bilionea Gautam Adani ambaye Kafulila anataka kumpa shirika la TANESCO ashitakiwa kwa utapeli huko Marekani
Hofu yangu. Wanakimbilia mahakama za kimataifa tukivunja mikataba. Na wanashinda na kuendelea kulipwa billions hata kama tutasitisisha huduma. Kama IPTL downs, buzwagi nk
 
Ingekuwa inaendeshwa kwa Sheria na Taratibu basi hizi pesa ambazo tunalipa kila siku kwa kushindwa Kesi sababu ya kuvunja mikataba kama hii ya Mangungo wa Msovero waliotuingiza kwenye hio Mikataba wangekuwa Lupango na sio Kuendelea kula Matunda ya Upuuzi wao...
 
Ingekuwa inaendeshwa kwa Sheria na Taratibu basi hizi pesa ambazo tunalipa kila siku kwa kushindwa Kesi sababu ya kuvunja mikataba kama hii ya Mangungo wa Msovero waliotuingiza kwenye hio Mikataba wangekuwa Lupango na sio Kuendelea kula Matunda ya Upuuzi wao...
Sasa unataka tuendelee kuvunja mikataba?
 
Sasa unataka tuendelee kuvunja mikataba?
Tusiingie kwenye Mikataba ya kipuuzi in the first place..., na Hizi Mahakama za Kimataifa ambazo zinaleta loopholes za corporations kuendelea kunyonya developing countries na kuharibu mazingira vifungu vibadilishwe au kwenye mikataba tusiende huko..., sababu kinachoendelea ni watu kuingia kwenye upuuzi wakijua wao na vikaragosi wao wasio wazalendo tutapelekana mahakamani ili wajilipe...

Ila kabla ya yote nilishauri hapa bila total 100 percent transparency kwenye mali ya UMMA tutaendelea kupigwa mpaka kesho (na wanaotupiga wala sio mataifa ya nje bali tunaodhani ni wenzetu humu humu nchini)

 
View attachment 3164291
=
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Bandari nchini Tanzania Bw. Plasduce Mbossa ameliambia The Citizens kuwa TANZANIA inaendelea na mkataba wake wa uendeshaji wa bandari na Kampuni ya Adani Group kupitia Gati No2.

Mtakumbuka Tanzania na Adani Groups wamesaini mkataba wa zaidi ya $95milioni karibu sawa na zaidi ya TZS 247bn wa kuendesha Gate namba 2 utakaodumu kwa miaka 30.

Wakati haya yanaendelea kwa upande wake Bw. Davidi Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa PPP yeye ameendelea kuwa kimya juu ya ama ataendelea na mpango wake wa awali wa kumpata mbia katika Ujenzi wa msongo wa Umeme pamoja na Uendeshaji wa Viwanja vya ndege kwa sharti la PPP kwa kupitia watia nia waliopo au laa.

Wakati huu ambapo Adani Green Energy Ltd pamoja na kampuni ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP zimeonesha nia hiyo ambazo ndizo kampuni pekee za kigeni zilizoonesha nia ya kuwekeza katika miradi hiyo na kwa kuzingatia tuhuma za sasa za rushwa na Ulaghai dhidi ya billionaire Adani Gautam.

Kumbe huyo ndio tuliambiwa ni DP World? Tumekwishaa. wavunje haraka kabla hawajapatwa na kashfa zaidi.
 
Duh!

Kiukweli ipo siku hawa wanasiasa wetu atatokea kiongozi mwingine kama JPM atawanyonga wote-tuanze upya! Huwezi ukawa na akili au nia njema na watu wako ukafanya maamuzi kama haya! No way.
Mtu pekee wa kusafisha UCHAFU huu ni Kassimu Majaliwa!!!
 
Serikali ya CCM haijazoea kitu kinaitwa uwajibikaji...
 
Back
Top Bottom