Tanzania kujenga viwanja 6 vipya bora vya mpira kabla ya 2026

Na sisi huku Mafia mtujengee kimoja, hatuwezi kuwa tunapanda maboti kuja kuangalia mechi huko kila mara.
 
mega projects za Egypt ni kama zipi?
 
Dodoma kinajengwa kiwanja cha watu 90,000 kwa masaada toka morocco
ilikuwa iwe 60,000 ila aliyekuwa katibu mkuu ndugu said yakubu alisema serikali ilifanya utafiti ya watu wanaoingia viwanjani kutazama mpira kwa mechi nyingi hawazidi 30,000 hivyo serikali iliamua msaada wa mfalme wa morocco utumike kujenga viwanja viwili (arusha na dodoma) na serikali itaongeza fedha ili miradi hiyo ikamilike.
 
Watanzania hawajui mpira.
Simba na Yanga zinafaulu sababu ya kuwekeza kwa wachezaji nje ya Tanzania
 
Duh,una uhakika hizi project hazina faida kiuchumi?

Ndio nyie mnaolalamikia kampuni za kubet huku ndio zinazoingiza pato kubwa la nchi
 
VIWANJA KWAAJILI YA KUTUPUMBAZA NA BURUDANI ZA SIMBA NA YANGA TUSIWAZE UKOSEFU HUDUMA ZA KIJAMII, SASAHIVI KILA HUDUMA YA KIJAMII NI MBOVU (UMEME,MAJI,USAFIRI N.K) NA STILL WANAANGAIKIA VIWANJA VYA MPIRA KWELI!!!?

WANANCHI INABIDI MUAMKE
 
wameshindwa kulipa fidia JNIA eneo la kipunguni. ahadi hewa hizo
 
Pesa zetu zimekosa kazi badala ya kuwekeza maeneo muhimu,utadhani tunahitaji sana burudani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…