Tanzania kujifunza Qatar kuondoa msongamano wa magari

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Serikali ya Qatar kwa mafanikio makubwa ya matumizi ya teknolojia ya kisasa na nishati safi katika mifumo ya usafiri wa umma.

Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo leo, Jumamosi, Septemba 26, 2026, jijini Doha, Qatar, mara baada ya kupokea taarifa rasmi ya uendeshaji wa kampuni ya usafirishaji ya Mowasalat kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani.

Waziri Mkuu, ambaye yuko nchini humo kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku tatu, amesema ubunifu na mifumo ya usafiri wa umma ya Qatar imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa magari barabarani kutokana na kuwa na usafiri wa uhakika.

“Nyumbani tunalo tatizo la msongamano wa magari na kupitia teknolojia mnazotumia, Tanzania inaweza kujifunza mbinu mlizotumia ili nasi tuweze kukabiliana nalo,” amesema Dkt. Nchemba.

Aidha, amebainisha kufurahishwa kwake na uamuzi wa kampuni hiyo kutumia nishati safi kwa sehemu kubwa, akihusisha hatua hiyo na ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi barani Afrika, jambo litakalosaidia maandalizi kuelekea michuano ya AFCON 2027.

Katika upande mwingine, Waziri Mkuu ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa ajira kwa Watanzania 722 katika nafasi mbalimbali, akisisitiza kuwa ni fursa nzuri kwa vijana wa Kitanzania kupata ujuzi na kujifunza teknolojia mpya.

Awali, Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani, alimweleza Waziri Mkuu kuwa Mowasalat inatoa huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia mabasi, teksi, na usafiri wa wanafunzi au matukio maalumu. Alibainisha kuwa kwa mwaka 2025, kampuni hiyo ilihudumia watu milioni 42, huku asilimia 70 ya magari yake ikitumia umeme na yakiwa yamefungwa mifumo ya ukaguzi wa kielektroniki kubaini hitilafu kwa haraka.
IMG_6223.jpeg
 
Pesa ndio kila kitu
Kama unakula hela zote zilizowekwa kwa ajili ya shughuli zake basi usitafute mchawi
Qatar ni nchi ndiogo sana na wametengeneza mpaka artificial island katikati ya Doha
Wana usafiri unaitwa Doha metro ni wa chini ya ardhi ambao hauhitaji dereva ni auto kwenda mbele inajiendesha yenyewe

Ingawa wazawa hawatumii ila foreigners wengi ndio usafiri wao
Yaani ni kama mapambo tu
Watu wana hela sana na wamewekeza
Sasa utawaiga una hela za kuwekeza na ku maintain matengenezo ya kila siku
Qatar kweli?
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Serikali ya Qatar kwa mafanikio makubwa ya matumizi ya teknolojia ya kisasa na nishati safi katika mifumo ya usafiri wa umma.

Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo leo, Jumamosi, Septemba 26, 2026, jijini Doha, Qatar, mara baada ya kupokea taarifa rasmi ya uendeshaji wa kampuni ya usafirishaji ya Mowasalat kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani.

Waziri Mkuu, ambaye yuko nchini humo kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku tatu, amesema ubunifu na mifumo ya usafiri wa umma ya Qatar imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa magari barabarani kutokana na kuwa na usafiri wa uhakika.

“Nyumbani tunalo tatizo la msongamano wa magari na kupitia teknolojia mnazotumia, Tanzania inaweza kujifunza mbinu mlizotumia ili nasi tuweze kukabiliana nalo,” amesema Dkt. Nchemba.

Aidha, amebainisha kufurahishwa kwake na uamuzi wa kampuni hiyo kutumia nishati safi kwa sehemu kubwa, akihusisha hatua hiyo na ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi barani Afrika, jambo litakalosaidia maandalizi kuelekea michuano ya AFCON 2027.

Katika upande mwingine, Waziri Mkuu ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa ajira kwa Watanzania 722 katika nafasi mbalimbali, akisisitiza kuwa ni fursa nzuri kwa vijana wa Kitanzania kupata ujuzi na kujifunza teknolojia mpya.

Awali, Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani, alimweleza Waziri Mkuu kuwa Mowasalat inatoa huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia mabasi, teksi, na usafiri wa wanafunzi au matukio maalumu. Alibainisha kuwa kwa mwaka 2025, kampuni hiyo ilihudumia watu milioni 42, huku asilimia 70 ya magari yake ikitumia umeme na yakiwa yamefungwa mifumo ya ukaguzi wa kielektroniki kubaini hitilafu kwa haraka.
View attachment 3678420
 
Attachments

  • 6405238-eae1ceee959bf6fd97d9fb2eab102cc4.mp4
    9.2 MB

mnh, juzi Italy, leo Qatar, wengine wanatalii mitaa ya NY!
 
Hawezi kutumia AI au youtube hadi aende mwenyewe?
 
Back
Top Bottom