Poverty ni moja ya sababu lakini sio tu poverty pia upumbavu wa wakazi wa eneo husika.Kwa hapa Tanzania miji yote ni slums (Naombeni radhi kwa ambaye atalipokea vibaya).
Miji yote na majiji yote yana mipangilio mibovu, huduma mbovu za kijamii.Nakupeni mfano halisi, DSM kwa Tanzania ndio sehemu ambayo mtu akiwa anaeleza ustarabu wa makazi kwa mtanzania lazima aitaje. Angalia mji wako, nenda kwamfano Mlimani city ambayo ni sehemu imekuepo siku nyingi na imekuwa ikipata wageni wengi wa ndani na nje ya Tanzania.
Kitu kinachoshangaza ni kuwa eneo lile ukishatoka tu kwenye uzio wake unakutana na takataka za kila namna angalia ile barabara kabla ya kufika rufungila uchafu mtupu. Chukua njia ya survey, hapo kidogo siku hizi wanajitahidi baada ya kuwekwa jengo la Sky City nadhani lakini before ilikuwa uchafu mtupu.
Nenda hiyo sijui posta ndo kabisa ujinga,inafika wakati unashindwa kuelewa kwamba huu ni umaskini au upumbavu. Ndio bado namba nzuri vipato vyetu ni vya chini hatuwezi sema tujenge makasri lakini hata mipangilio imetushinda?I suggest poverty shouldn't mentioned but ignorance