Tanzania kununua injini za disel kuendesha SGR

BabaMia

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
270
Reaction score
554
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanzisha mpango wa kununua injini za dizeli ili kuhakikisha huduma ya usafiri wa reli ya kisasa (SGR) bila kikwazo endapo umeme utakatika.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, amethibitisha hilo na kuelezea kuwa tayari kampuni moja imebainishwa kuzalisha injini hizo.

Huduma ya reli kutoka Dar hadi Morogoro imekuwa ikikumbwa na changamoto ya umeme mara kadhaa na kusababisha abiria kukwama safarini kabla ya kufika wanakokwenda.

1734079419942.jpg
1734079437562.jpg
1734079445424.jpg
 
Hivi wakinunua ma generator hayawezi kufua umeme ukatosha??
 
Ila wanangu nishati ya mafuta bado haikwepeki mpk miaka 100 tangu sasa,,
Fikiri tesla, n.k ktk gari zao betry zikiisha umeme wanawasha jenereta kuzipa power.
Umeme completely bado ni muhogo mchungu.
 
Ni kupunguza matumizi ya mafuta ila sio kuondoa
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanzisha mpango wa kununua injini za dizeli ili kuhakikisha huduma ya usafiri wa reli ya kisasa (SGR) bila kikwazo endapo umeme utakatika.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, amethibitisha hilo na kuelezea kuwa tayari kampuni moja imebainishwa kuzalisha injini hizo.

Huduma ya reli kutoka Dar hadi Morogoro imekuwa ikikumbwa na changamoto ya umeme mara kadhaa na kusababisha abiria kukwama safarini kabla ya kufika wanakokwenda.
Wanaturudisha kulekule kwenye kula moshi njia nzima...
 
Wenye biashara zao za mafuta Msoga na genge lake tayari wameishaona upenyo! Kwanini wasiweke mfumo gesi kama mbadala wa umeme,
Eti nishati Safi ya kupikia, kampeni ya mama, kwanini sio nishati Safi ya kuendesha treni?
 
Utasikia wakimshukuru mama yao na kudai anaupiga mwingi, raha sana kuwaongoza mazezeta.
 
Wenye biashara zao za mafuta Msoga na genge lake tayari wameishaona upenyo! Kwanini wasiweke mfumo gesi kama mbadala wa umeme,
Eti nishati Safi ya kupikia, kampeni ya mama, kwanini sio nishati Safi ya kuendesha treni?
Hiii plan ni sahihi kbsa , sasa either haiwez kuendeshwa na Gesi.

Dunia ya sasa ninGesi na umeme
 
Tunaviongozi matapeli sana awamu hii ya mama.Mwanzo huyu masanja alitudanganya watz kuwa ikitokea umeme umezima treni itaendelea Kwa muda wa kama saa Moja na nusu lakini kumbe ilikuwa uongo mtupu.sasa hivi wanaturudisha Tena treni la diseli ambalo baadae Tena litakufa kabisa kama lilivyokufa kabisa kipindi Cha rais fisadi kikwete alipowapa wahindi Kwa sababu zake za kijinga kuwa eti ni wawekezaji!
 
Kama tatizo ni umeme basi wa focus na kutatua hilo tatizo la umeme iyo pesa iliyotengwa ielekezwe kwenye kutatua shida ya umeme.

Kitendo cha kufikiria mbadala wa nishati katika mfumo wa nishati ya umeme ni kudhihilisha kwamba wamefeli/wameshindwa kusimamia mradi na nikukwepa majukumu...

Ili kusonga mbele na kufanikiwa katika usimamizi na uendeshaji ni lazima kukabiliana na changamoto husika kumkwepa hakutatui /kuondoa tatizo.

Kwanza tulikubaliana kua train zitakua na betri pindi ikitokea hitilafu, pili kama hakuna huo mfumo wa betri wangetafuta namna yakudesign mfumo wa betri na sio kutafuta engine za mafuta.
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanzisha mpango wa kununua injini za dizeli ili kuhakikisha huduma ya usafiri wa reli ya kisasa (SGR) bila kikwazo endapo umeme utakatika.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, amethibitisha hilo na kuelezea kuwa tayari kampuni moja imebainishwa kuzalisha injini hizo.

Huduma ya reli kutoka Dar hadi Morogoro imekuwa ikikumbwa na changamoto ya umeme mara kadhaa na kusababisha abiria kukwama safarini kabla ya kufika wanakokwenda.
Tenda ya kujaza dizeri kama namuona kikwete au rostam
 
Hesabu ni fupi tu ni hivi,
Kuna watu kazi yao ni kutengeneza matatizo ili wanufaike kupitia hayo matatizo, Hesabu ya gharama ya hiyo diesel tayari ina mtu wake humohumo ambaye ndo chanzo cha hilo tatizo.
 
Back
Top Bottom