Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Baadhi ya Nukuu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika.
“Tanzania ni moja ya Nchi 12 zitakazozindua mpango mahususi wa kitaifa kuhusu nishati”
“Kupitia mpango wetu tunatarajia kuongeza kasi ya kuunganisha umeme nchini hadi kufikia 72% ifikapo mwaka 2030, ili kufanikisha azma hiyo ndani ya muda wa miaka mitano ijayo, tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 13, ambapo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi hapa nchini.”
“Kupitia mpango huu tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko”.
“Tanzania ni kiungo muhimu katika kuunganisha umeme Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na hivyo kuwezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Misri, tayari tumeunganisha miundombinu ya umeme na Nchi za Burundi, Kenya na Rwanda na sasa tunaendelea kuunganisha miundombinu ya umeme na Nchi ya Zambia na Uganda”
“Kuwepo kwa miundombinu hiyo kutawezesha biashara ya nishati kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme ikizingatiwa kuwa hadi November 2024 mahitaji ya umeme Tanzania yalikuwa megawatt 1888 wakati uzalishaji wetu mi megawatt 3431”
“Muelekeo wetu ni kufikisha umeme katika vitongoji vyote 64359 baada ya kufanikiwa katika vijiji vyote vya Tanzania, hadi sasa tumevifikia vitongoji 32827 na kazi inaendelea katika vitongoji vilivyobakia , la nne ambalo mpango huu utafanya ni kusambaza nishati safi ya kupikia”
🇹🇿Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika
🗓️28 Januari, 2025
📍JNICC - Dar es salaam