Tanzania kupeleka timu nne michuano ya CAF kwa mwaka 2020/21

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Baada ya Klabu ya Simba kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na timu ya Gor Mahia kutolewa katika michuano ya Shirikisho, Tanzania imefika nafasi ya 12 kutoka ya 24 kwenye viwango vya ubora Afrika

Kutokana na Tanzania kufikia nafasi hiyo, kwenye michuano ya CAF kwa mwaka 2020/21 timu mbili zitashiriki kwenye michuano ya Klabu Bingwa na mbili zitashiriki michuano ya Shirikisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaona vyura wanavyopita kimya kimya kwa aibu... Watu walipokuwa wanapaza sauti Tanzania nzima kuishangilia SIMBA SC A.K.A MNYAMA MKALI, Nyie mlikuwa mnahama vituo vya kushangilia upinzani na kwa sababu ya ujuha wenu hamkujua kwamba kufanya kwetu vizuri ilikuwa njia nzuri ya kuwarudisha na nyie katika ramani ya soka... Haya ndio matokeo ya kufanya vizuri kwa Simba. Nchi imepata heshima tena Africa...
 
Huu Ni msimu gani wa Caf?
Ni 2019/2020
au Ni 2018/2019?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu Ni msimu gani wa Caf?
Ni 2019/2020
au Ni 2018/2019?

Sent using Jamii Forums mobile app

Huu ni msimu wa 2018/2019... Msimu wa 2019/2020 Timu zitaenda 2 kama kawaida na kwa msimu huo wa 2019/2020, Nchi inakuwa na muda mzuri wa kuweka utaratibu mzuri wa kupitisha timu 4 kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2020/2021 wa CAF. Msimu wa 2018/2019 ndio unaishia, hivyo huwezi kupata timu 4 kwa haraka bila utaratibu ili timu ziende 4 msimu wa 2019/2020. CAF waliliona hilo ndio maana walisogeza msimu mmoja zaidi ili kuwe na utaratibu maalum wa kupata hizo timu 4.

Kama nitakuwa nakosea, naomba nirekebishwe....
 
Vyura hata kusema asante mnashindwa..! Au mnaona aibu[emoji23]

Ole wenu mkafungwe hovyo hovyo na kushindwa kufikia hata makundi ilhali tumewabeba kwa hisani tu

Na mkumbuke mwakani CL tunarudi tena na nguvu mpya [emoji23][emoji23][emoji23]
 
SIjaona cha kusheherekea, mana hizo timu 4 zitakwenda kwa msimu mmoja utaofata mbele zitarudi mbili kama kawaida.
Mana haya yaliotokea safari hii musitarajie kama ndio yatakua ya kila siku.
 
Umeona Uzi huuu Shadeeya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyura hata kusema asante mnashindwa..! Au mnaona aibu[emoji23]
Ole wenu mkafungwe hovyo hovyo na kushindwa kufikia hata makundi ilhali tumewabeba kwa hisani tu
Na mkumbuke mwakani CL tunarudi tena na nguvu mpya [emoji23][emoji23][emoji23]
AIBU waliyonayo niya kushikwa unalamba debe ukweni... Ila watake au wasitake Simba sio level yao.
 
Iwapo Simba asipochua ubingwa atakuwa kajibeba mwenyewe
 
Hongereni jamani.
Subirini zamu yenu kubebwa mwakani.
No situation is permanent.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…