Kwa kumbukumbu zangu hawa watu walivamnia Tanzania wakati wa uchaguzi 2020 na pia kufanya mauaji na kilichofanyika ni operesheni ya kuwasaka kwenye misitu ya ndani na na maeneo ya ndani ya msumbiji karibu na mpaka wetu na wakishirikiana na msumbiji na pia kwa mujibu wa siro alisema walikuwa na ushirikianoano na baadhi ya watanzania maana walichunguza kugundua walikuwa wanachoma nyumba na baadhi kwa makusudi wanazi ruka hatahivyo ambacho hakiongelewi ni kuwa baada kifo cha Magu nadhani misimamo ama sera ya Serikali ni kama imekuwa tofauti
Mkuu 'gataca', kuna jambo hapa ambalo sio la kawaida, na huyu 'Janja', anayejifanya kueleza inaelekea hana kitu anachokielewa, lakini anataka watu tudhani anajuwa kitu, kumbe hana lolote!.
Jambo lisilo la kawaida ni kusikia Waziri wetu Liberata Mulamula akisema pafanyike mazungumzo, hili siyo jambo la kawaida.
Jambo lisilo la kawaida ni kusikia Wizara yetu ya Mambo ya nchi huko siku za nyuma ikitataa ushiriki wetu ndani ya SADC katika kuwasaidia Msumbiji, lakini miezi kadhaa tunajikuta tunabadili msimamo huo!
Haya siyo mambo yaliyozoeleka kwa nchi yetu hii ya Tanzania ambayo historia yake inafahamika kwa misimamo thabiti kwenye maswala kama haya.
Linaloshangaza zaidi ni kwamba hawa magaidi mwanzo wao/wanakotokea ni kama panafahamika vyema, na uhusika wetu na wao ni kama unajulikana vizuri. Sasa maana ya kujichanganya huku kwa serikali yetu sababu yake kuu ni nini hasa?
"Janja' anazungumzia mambo hapa kama mlevi fulani tu, na wala hajibu hoja yoyote inayowasilishwa kuijibu.
Binafsi sina shaka yoyote na uwezo wa vijana wetu kuwakabili hawa magaidi kama wakiamuriwa kufanya kazi hiyo, iwe humu humu ndani kwetu au huko Msumbiji. Tatizo ni hili la mikanganyiko inayowekwa na serikali.
Hatuwezi kuwa nchi ya kuanza kuangalia vinchi kama Rwanda wanafanya nini, halafu ndio na sisi tuanze kujitetea au kudanganya watu kwamba tumefanya makubwa huko, ambayo ushahidi unaoonekana ni kwamba hakuna tulichofanya huko, maanake tungekuwa tumefanya, Rwanda wasingekuwa na sababu ya kwenda huko na kujitangazia kazi kubwa waliyofanya katika muda wa wiki moja tu baada ya kuwasili huko!
Sure thing
je, sadc mission ni sustainable?
maana naskia jamaa wameshavuka na kurudi huku kwetu na wanajipanga upya
Unaona jinsi ulivyo 'bogus' wewe!
Hivi hata chembe ya aibu kichwani mwako huna?