Tanzania kupeleka washiriki 7 tu kwenye mashindano ya Olympics 2016

Bolt, Raia wa Jamaica ashinda tena medali ya dhahabu, alipata ushindi huo wa kipekee alipokimbia akitumia muda wa sekunde 9.58, na kukaribia mno kuivunja rekodi ya dunia. Alifuatwa na Mmarekani Justin Gatlin aliyechukua medali ya fedha huku nambari ya tatu ikitwaliwa na Adress de Gresse wa kutoka Canada. Umati mkubwa uliokusnyika katika uwanja mmoja nchini Jamaica ulishangilia kwa shangwe na vigelegele punde tu Bolt alipomaliza mbio hizo. Pia Jemimah Jeptoo Sumgong aliipatia Kenya medali ya kwanza ya dhahabu baada ya kushinda mbio za marathon kwenye mashindano hayo. Hiyo pia ilikuwa medali ya kwanza ya Kenya katika marathon ya wanawake katika michezo ya Olimpiki. Vilevile Sumsong mwenye umri wa miaka 31, alimaliza mbio hizo kwa saa mbili, dakika 24 na sekunde nne, na kumshinda Eunice Kirwa wa Bahrain aliyechukua medali ya fedha. Nafasi ya tatu ilimwendea Muethiopia Mare Dibaba.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda akishirikiana na Chama Cha waogeleaji Tanzania, wamefanya mapokezi ya vijana walioiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Olympic huko Rio De Janeiro, licha ya Tanzania kutofanya vizuri kwenye mashindano yanayoendelea huko Brazil. Hilal Hemed Hilal aliogelea Alhamis tarehe 11/08/2016 katika heat namba 4 freestyle na kuweza kushika nafasi ya kwanza kwa kutumia sekunde 23:70. Ingawa hakupata nafasi ya kusonga mbele, matokeo hayo ni makubwa na ni rekodi ya juu tangu timu ya Tanzania ianze kushiriki mashindano ya Olympic.... Inshallah may be next time wa tz tutarudi na medali ya bati tusife moyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…