Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA SABA WA (7) WA JUMUIYA YA MAMLAKA ZA USIMAMIZI WA USAFIRI MAJINI AFRIKA
Dodoma.
Wizara ya Uchukuzi inautaarifu umma na wadau wa sekta ya usafiri majini kuwa Tanzania kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeteuliwa kuwa nchi mwenyeji wa Mkutano wa Saba (7) wa Kimataifa wa Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri Majini Barani Afrika, utakaofanyika kuanzia tarehe 29 Novemba hadi 01 Desemba, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Lengo la mkutano huu ni kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya udhibiti na usimamizi wa usalama wa usafiri majini barani Afrika huku kipaumbele kikiwa ni mustakabali wa usafiri wa majini na kuongeza ushirikano baina ya nchi wanachama
Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Kuimarisha mustakabali wa sekta ya usafiri majini barani Afrika: Ushirikiano katika Teknolojia na Ubunifu ili kupunguza hewa ukaa, kuimarisha usalama, na mazingira ya sekta ya usafiri majini kwa mustakabali endelevu"
Mkutano huo utatumika kama jukwaa muhimu katika kuwezesha wadau kushiriki katika majadiliano yanayogusa masuala ya teknolojia na ubunifu yenye kulenga katika kuimarisha usalama na mazingira ya usafri majini, pia, watapata fursa ya kuingia makubaliano ya kibiashara pamoja na kuanzisha mitandao na ushirikiano katika uendeshaji masuala mbalimbali yanayohusiana na fursa za uchumi wa buluu.
Mkutano huu wa kihistoria utafunguliwa rasmi na Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Bahari Duniani (MO), Bw. Antonio Dominguez pamoja na wataalam wa usafiri majini, viongozi wa mamlaka za udhibiti wa usafiri kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, zipatazo 50 ambazo zina bahari, maziwa na mito na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya Kimataifa.
Ushiriki wa Bw. Dominguez ni heshima kubwa kwa Tanzania hasa kipindi hiki tunapotekeleza Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu, ambapo kama nchi tumebainisha masuala ambayo Serikali kwa kushirikiana na wadau, kuhakikisha nchi inanufaika na fursa zitokanazo na rasilimali za Uchumi wa Buluu ili kukuza uchumi wa Taifa kwa maendeleo endelevu.
Aidha, Tanzania itaendelea kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta ya usafiri kwa njia ya Maji zinazohusiana na utumiaji wa rasilimali za bahari na maziwa pamoja uchukuzi ili kukuza uchumi wa buluu, kufanya tafiti na kuwekeza katika uvunaji wa rasilimali bahari na maziwa Zitakazosaidia kuongeza UweZo wa endelevu Serikali kuwahudumia wananchi na kuwaleta maendeleo
Tunatoa wito kwa wadau wote wa sekta ya usafiri maiini, wakiwemo wasafirishaj, wamiliki wa vyomnbo vya usafirishaji majini, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, viongozi wa Serikali kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huu muhimu ili kuunga mkono juhudi za Serikali Katika kuimarisha usafiri wa majini hapa nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Katika Mkutano huo pia kutakuwa na maonyesho na utoaji elimu kwa umma na washiriki watakao ehiriki katka mkutano huo, hivyo tunawakaribisha wananchi wote