Tanzania kupitia TRA ianze kufuata uchumi halali kuondosha malalamiko ya wafanyabiashara na kukuza uchumi

Tanzania kupitia TRA ianze kufuata uchumi halali kuondosha malalamiko ya wafanyabiashara na kukuza uchumi

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Malalamiko ya hali mbaya za kiuchumi na kutoka kwa wafanyabiashara yamekuwa sugu. Njia zote kuleta nafuu zimeshindikana.Sababu ya hali hiyo ni kwa vile njia za uchumi zinazofuatwa si halali.

Tumezoea kurithi kila tunacholetewa kutoka kwa watu wa Ulaya waliowahi kuwa wakoloni wetu.Na kwa vile elimu zetu nazo zinafuata mikondo yao si rahisi kuamini kuwa tunaweza kupata suluhisho au nafuu ya matatizo yetu kwa kufuata mifumo mingine tofauti na yao.

Kwa ufupi tuna nafasi nzuri ya kuondosha kero hizo na uchumi kukua na huku kila mmoja akilipa kodi kwa kuridhika kwa njia ya kufuata uchumi wa kiislamu.

Machache ambayo tunaweza kuyataja hapa ambayo ni tofauti na tunavyofanya sasa ni kama nitakavyoainisha hapo chini.Upana wake unapatikana kutoka kwa wasomi ambao wamejaa kila sehemu ya uchumi huo halali.

Kodi hatoleshwi mfanyabiashara kabla ya kufanya hiyo biashara na kupata faida.Kwa sasa huwa mfanyabiashara anafanyiwa makadiria makubwa alipe kabla ya shughuli yoyote.Akishindwa kulipa kunakuwa na vitisho vikali sana vinavyowanyima watu utulivu.

Kama utaratibu huo ukitumika basi biashara nyingi hazitolazimika kupata bughudha za kulipa kodi na badala yake wako wengine watakaopewa mitaji kukuza biashara hizo kutoka kwa kodi zilizolipwa kihalali kutoka kwa wanaostahiki kulipa

Mamlaka ya mapato itakuwepo na mahesabu yatatunzwa na hata nguvu ikibidi kwa wakwepa kodi pia itatumika lakini kila kitu kitakuwa halali na hata aliyekwepa kulipa ataridhika na adhabu atakayopewa au atalipa kama inavyotakiwa.
 
Back
Top Bottom